ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, December 21, 2012

Wasanii wakongwe wampongeza Rais Kikwete kwa kuwajali.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea ujumbe wa wasanii wakongwe wa muziki wa dansi pamoja na filamu
uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam kumpongeza  kwa kuwajali wasanii wa aina zote na hata kuamua kutoa tuzo kwa wasanii ambapo mwaka huu amewatunuku Muhidin Maalim Gurumo na Hayati Marijani Rajabu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mwamuziki Waziri Ali wa kundi la Kilimanjaro Bendi Wananjenje.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na ugeni wake.
Mwanamuziki Mkongwe King Kiki a.k.a Mzee wa Kitambaa Cheupe akisalimiana na Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Serikali imeanza kutoa Nishani kwa wasanii kwa vile inatambua umuhimu wao katika jamii.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaeleza wawakilishi wa sanaa mbalimbali nchini waliofika Ikulu leo asubuhi kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kuwatambua na kuwapa heshima kubwa ya Tuzo na Nishani wasanii katika siku ya sherehe za Uhuru za tarehe 9 Disemba, Ikulu, Dar-Es-Salaam.
“Tumetoa Nishani kwa vile wasanii wanatoa mchango mkubwa, tumeanza kutoa nishani mwaka huu na tutaendelea kutoa miaka ijayo kwani kwa kuitambua sanaa, mnawapa moyo wasanii kuendelea kujituma na kuwa wabunifu zaidi” Rais amesema na kuongeza, “Tumeingiza Nishani ya Wasanii na Watafiti maana nao wanafanya kazi kubwa sana ya kutafiti mazao na mbegu mbalimbali ambazo zinaongeza tija katika kilimo nchini”.
Katika kumbukumbu ya kusherehekea miaka 51 ya  Uhuru wa Tanzania bara mwaka huu, Rais Kikwete alitunuku nishani kwa makundi mbalimbali ya watu waliotoa mchango mkubwa katika jamii na waliotumikia taifa kwa uadilifu.
Rais alitoa Nishani ya Sanaa na Michezo kwa mara ya kwanza kwa wasanii nchini ambapo Bi. Fatma Baraka Khamis (Bi Kidude) kupitia Baraza la Sanaa Zanzibar, Kiongozi wa Muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma Muhidin Gurumo, Kiongozi wa Zamani wa Bendi ya Dar Intrenational Marehemu Marijan Rajab walipata tuzo hiyo.
Wengine ni Msanii wa maigizo na filamu nchini Marehemu Fundi Said (Mzee Kipara) na Mwanariadha mkongwe John Steven Akwari.
Rais amewataka wasanii kushirikiana na serikali lakini pia wawe mstari wa mbele katika kupigania haki zao na sio kusubiri serikali tu iwafanyie hivyo.
Wasanii hao wamefika Ikulu wakiongozwa na Bw. Ruge Mutahaba wa Clouds Media Group.
Wengine ni Addo Mwasongwe, Rais wa Shirikisho la Muziki na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Injili, Bw. Juma Ubao Mwenyekiti wa Chama cha Muziki Tanzania (CHAMUDATA).
Bibi  Shakila Said, Mkongwe wa Muziki wa Taarab Nchini, Bi Carola Kinasha Msanii wa Muziki , Mzee King Kiki msanii wa Muziki wa Dansi Mwana FA, msanii wa Kizazi Kipya na Bw. Waziri Ally , msanii wa Muziki.
Wawakilishi hao pia wamemshukuru Rais kwa msaada wa hali na mali anaotoa kwa wasanii mbalimbali wanapopata matatizo ambao hivi sasa wapo katika hatua mbalimbali za matibabu ya afya zao hapa nchini na nchi za Nje.
“Haya mengine ninayafanya tukama wajibu wa  kibinadamu kwa vile nina nafasi ya kufanya hivyo na pale tunapokua na uwezo tunasaidia kama binadamu wenzetu” Rais Amesema. 
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu – DSM
21 Desemba, 2012

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...