Waziri
Mkuu wa Mali Cheik Modibo Diarra ametangaza kujiuzulu wadhfa wake
katika televisheni ya taifa, saa chache baada ya kukamatwa na kuwekwa
chini ya ulinzi na wanajeshi wanaosadikiwa kuhusika na mapinduzi
yaliyofanyika mwezi Machi mwaka huu.
Cheik
Modibo Diarra alikamatwa nyumbani kwake katika mji mkuu wa Bamako, kwa
kile kinachosemekana kuwa ni maagizo ya Kiongozi wa Mapinduzi hayo
Kapteni Amadou Sanogo.
Waziri Mkuu huyo alikuwa akijiandaa kusafiri kuelekea Ufaransa.
Diarra
alikamata madaraka ya Uwaziri Mkuu wa Serikali ya Mpito mwezi Aprili
baada ya maafisa wa jeshi waliofanya mapinduzi kukabidhi madaraka
mikononi mwa raia.
No comments:
Post a Comment