Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na msafara wake, wakikaribishwa na viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma baada ya treni kutoka Dar es Salaam, kuwasili leo asubuhi mjini Kigoma, Wanaoshuka ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma. (Picha na Bashir Nkoromo).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose  Migiro (kushoto) wakisindikizwa baada ya kushuka kwenye treni mjini Kigoma, ambako waliwasili leo wasubuhi wakitoka jijini Dar es Salaam.Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Mamia ya wananchi wakiwa wamejitokeza kupokea msafara wa Kinana ulipowasili kwa treni Stesheni ya Kigoma leo asubuhi. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokewa kwa ngoma kwenye stesheni ya Kigoma, alipaowasili kwenye stesheni hiyo na ujumbe wake akitokea jijini Dar es Salaam. Wapili ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Walid Kaborou na kulia ni Nape akishiriki kupiga ngoma. 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshukuru dereva wa treni Kambi Ali, baada ya treni ya abiria aliyoendesha akiwemo Kinana na ujumbe wake kuwasili mjini Kigoma leo asubuhi. Wengine Wapili kushoto ni Dk. Asha Rose Migiro na Nape Nnauye
Kinana akisalimiana na wananchi kwenye stesheni ya Kazuramimba leo saa 12, asubuhi. ngoma. Kinana na ujumbe wake wamesafiri kwa treni hadi Kigoma kwa ajili ya sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Februari 3, 2013 mjini Kigoma. 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akimfurahia mtoto Ali Saidi mwenye umri wa miezi minane, ambaye ni mtoto wa  mmoja wa abiria aliowakuta kwenye  Stesheni ya Kigoma, msafara wa Kinana ulipowasili leo kwa treni.
Mwananchi wa Kaliua akipeleka kupakia mchele kwenye behewa, treni ilipofika stesheni ya eneo hilo mkoani Kigoma leo.
Abiria kutoka Tabora kwenda Kigoma wakiwa katika behewa leo.
Kinamama wa Uvinza, wakipeleka kuuza chumvi kwa abiria, treni ilipofika kwenye stesheni ya eneo hilo la  Uvinza leo ikitoka Dar es salaam kwenda Kigoma