HALI SI SHWARI MTWARA GARI LA POLISI LACHOMWA MOTO NA INASEMEKANA NYUMBA YA MH HAWA GHASIA YABOMOLEWA MUDA HUU
Mwandishi wa habari aumia katika vurugu za kgesi
mtwara zinazoendela muda
Askari wa kutuliza ghasia wakiwa tayari kutuliza
fujo Mtwara kwa kile kilichoelezwa ni vurugu zinazoendelea za gesi
*************
VURUGU zinaendelea mjini Mtwara ambapo
kwa sasa wananchi wamechoma moto vyoo vya mahakama ya Mwanzo na kuvunja
vioo vya Nyumba ya Hawa Ghasia Waziri wa Tamisemi na Mohamed Sinani
Mwenyekiti wa CCM mkoa zilizopo mtaa wa Sinani.
Wakiwa katika mahakama ya mwanzo Polisi
walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba mawe na kufunga barabara zote
za kuingia na kutoka kituo kikuu cha mabasi na soko kuu, licha ya
kufyatua hewani mabomu ya machozi.
Baadhi ya barabara zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi……
Diwani Chehako akiwa nyumbani kwake
mwandishi wa Channel Ten, John Kasembe
POLISI
leo wamelazimika kupiga mabomu ya machozi kutwa nzima katika kata ya
Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani kutawanya wananchi
walioizingira nyumba ya diwani wa kata hiyo Mohamedi Chehako kwa madai
ya kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake, huku mwandishi wa habari
mmoja akiripotiwa kujeruhiwa.
Hii
ndio Ilikuwa Mahakama ya Mwanzo Mtwara ikimalizika baada ya kuchomwa na
Wananchi wa Mtwara waliokuwa wakizunguka kwa madai mbalimbali ikiwemo
Imani za Kishirikina za Diwani,Pamoja na sakata la gesi kwa njia ya
Mabomba kutoka Mtwara kwenda Kinyerezi..
Maaskari wakitulia ghasia
Mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuwasiliana na kamanda Nzuki kwa njia ya simu za mkononi hakuweza kupatikana.
Habari
ambazo hazijathibitishwa na kamanda wa polisi mkoani hapa, Maria Nzuki
zinadai kuwa majira ya saa 10 kasoro za jioni watu wanaodaiwa kuwa ni
wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliingilia kati na
kuanza kutembeza mkong’oto kwa wananchi ili kuzima vuguvugu hilo.
Wananchi
walitoa tuhuma hizo baada ya kukuta ungo ikiwa na tunguri ndani yake
ambayo inadaiwa kuwa ni ndege ya wachawi uwanjani kwake maeneo ya
makabuli Msafa.
Wananchi
walijikusanya nyumbani kwa diwani huyo na kumshinikiza awatoe wachawi
nje ili waweze kuwadhibu, amri iliyopingwa na diwani huyo.
Kadri
mda ulivyokwenda ndivyo wananchi walivyozidi kuongezeka na hatimaye
kulijitokeza kundi la watu walioanza kutia vurugu, hali iliyomlazimu
Chehako kuomba msaada wa polisi.
Mashuhuda
wa tukio walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa polisi walipofika
waliwasihi wananchi kutawanyika kwa kuwa ungo na tunguri zake zilikuwa
zimeteketezwa kwa moto na diwani huyo mbele ya wananchi hao.
“Wananchi
waliendelea kupinga na kudai ndani ya nyumba kuna rubani na abiria wa
ndege nimewahifadhi…polisi wakawachagua wananchi watano na kuingia ndani
ya nyumba kuwasaka watu hao…hawakuona kitu, walitoka nje na kuwamabia
wenzao hata hivyo wenzao walibisha” alisema Chehako alihojiwa nyumbani
kwake.
Aliongeza
kuwa “walianza kurusha mawe nyumba…polisi walianza kupambana nao kwa
kuwarushia mabomu…hata hivyo wananchi walikuwa wanakimbia na kwenda
upande wapili kufanya vurugu”
Akihadithia
mkasa huo, Chehako alibainisha kuwa ni kawada yake kuamka alfajiri kwa
ajili ya sala ya asubuhi, lakini asubuhi ya jana alishindwa kuamka
mapema, hata hivyo hakuweza kuhisi jambo lolote.
“Ilipofika
saa 12 asubuhi nikaanza kusikia watu wakishangaa kitu nje, nilipotoka
nikakuta nyungo na tunguri ndani yake…mara wakaja vijana wawili na
pikipiki wakachukua ule ungo na kukimbia nao…nikawatuma vijana wawafuate
waurudishe…walifanikiwa na nyungo ile ilirejeshwa nyumbani hapa na
ndipo nilipouteketeza kwa moto” alisema na kuongeza kuwa “Nilidhani
yatakuwa yameisha, lakini wananchi waliendelea kudai nimewafungia
wahuska ndani, si kweli hakuna mtu humu ndani wala mimi sijui
kilichotokea hadi hivyo vitu vikawa humu ndani”
Katika
mapambano hayo ya wananchi na polisi, wananchi kwa kutumia mawe
wamemjeruhi Mwandishi wa Habari wa Channel Ten mkoani hapa, John Kasembe
kwa jiwe kichwani, sehemu za kisogoni ambapo ametibiwa zahanati ya
Fajima na anaendelea vizuri.
Kwa mujibu wa Kasembe alipigwa mawe kichwani akiwa kazini kukusanya habari na wananchi waliokuwa wakiwarushia mawe polisi.
Ofisa
wa polisi ambaye jina lake hakutaka litajwe kwa sababu si msemaji wa
jeshi hilo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa gari
moja ya polisi PT 1421 limevunjwa kioo cha mbele kwa mawe.
No comments:
Post a Comment