ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, January 26, 2013

MASASI NAKO HAKUKALIKI, VURUGU KUBWA WANANCHI HAWATAKI GESI ITOKE. GARI NA NYUMBA YA MBUNGE NA MAHAKAMA YA MWANZO VYATEKETEA KWA MOTO (The greatest wealth is to live content with little.)



 Gari la maji yakuwasha lahisiwa halina maji, askari walipanda wakashuka kulikimbia
 
Habari nilizozipata hivi punde kutoka Masasi ni kuwa maandamano yameanza tena na safari hii yanaongozwa na dereva boda boda ambao wameingia barabarani.
Risasi za moto na mabomu ya machozi yanapigwa kutawanya watu na tayari nyumba moja imechomwa moto. Gari la maji ya kuwasha limefika ila bado watu wanazidi kuongezeka
Tayari gari na nyumba ya mbunge imechomwa moto na vijanga wanazidi kusonga mbele wakiwa na madumu ya petrol
Mahakama ya mwanzo imechomwa moto na polisi wamejifungia ndani wanarusha mabomu ya machozi wakiwa ndani. Askari magereza wamejaribu kuwasha gari la maji ya kuwasha lakini bahati mbaya halina.maji hivyo wakashuka na kukimbia na wananchi wanataka kulichoma moto
 
(dalili za moto ni Moshi, tukisubiri moto uwake kuna mawili, kuweza kuuzima au kutoweza kuuzima. Hata hivyo si kila mtu anafurahia matunda haya, hivyo ni rahisi maadui wengi kuingia na kuleta mtafaruku mwa tayarikubwa. Kama bado hatujawa tayari kuwa na neema hii basi tuache. Kwani gesi inaoza jamani? Tuache watotot wetu wakasome miaka kama 20 hivi alafu waje waweke sera nzuri. kuna haja gani ya kufa kwa ajili ya mali. Ni nini kinaweza kununua uhai? Na watunga sera wakiwa na sera nzuri ambazo kila mtu atafaidika basi hakutakuwa na matatizo. Tangu wakati utafiti unaanza, wawekezaji wameingiza mitaji yao, kumbe hatukuwekeza kwa wananchi, kuwaelimisha, kuwashirikisha, sasa ni vigumu maana hata asiyejua gesi ni nini anapiga kelele. A library of wisdom, is more precious than all wealth, and all things that are desirable cannot be compared to it. Watunga sera na wananchi wa Mtwara, kaeni pamoja.


 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...