Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili
kwenye kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli tayari kwa hafla fupi
ya uzinduzi wa vikoba katika kijiji hicho.Katikati ni Mkewe Mama Regina
Lowassa aliefatana nae kwenye hafla hiyo ya Uzinduzi wa Vikoba.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe
Mama Regina Lowassa wakiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mswakini
Wilayani Monduli walipowasili tayari kwa hafla fupi ya uzinduzi wa
Vikoba katika kijiji hicho.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa
hotuba yake kwa wananchi wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli wakati
wa hafla ya uzinduzi wa VIKOBA kijijini hapo.Mh. Lowassa katika hotuba
yake,amesema kuwa ushirika wa VIKOBA ni sawa na mshipa wa damu kwa sera
ya maisha bora kwa kila Mtanzania,pia alisema kuwa kutokana na kutambua
hivyo ushirika wa Vikoba utaanzishwa katika wilaya nzima ya
Monduli.Maisha bora kwa kila Mtanzania ni sera aliyoingia nayo
madarakani Rais Jakaya Kikwete.
Afisa
Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli,Bi Judith (kulia) akikabidhi kwa
Mhe. Edward Lowassa hati maalumu ya uzinduzi wa Vikoba ili ikabidhiwe
kwa Wananchi Mswakini Monduli.
Baadhi ya wanachama wa Vikoba wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli.
No comments:
Post a Comment