ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, January 8, 2013

Msiba mkubwa Kenya

 
Tembo aliyekatwa shingo kwa ajili ya kutolewa meno
 
tembo aliyeuwawa
 
Tembo huwa wanakaa katika kundi moja na huwa wanakuwa ni uzao mmoja
  
Askari wa wanyamapori akimwangalia tembo aliyeko katika uzio
  
    
Picha mbali mbali za tembo waliouwawa
  
askari wa wanyama pori akiangalia mzoga wa tembo aliyeuwawa na majangili
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhu9tIk4hQeQjU_QzQPEikwW9xBQwCJ2ws42UQjndR8DHoucs4ptG_w0w-EbR8uL-A4IdQMAhYD8EUyWM6ssxfZ5Es337MUFAHuQQ4_7AIS-515OHysEiEh-JxvxKJzeqd_0MG2rAEANkzE/s1600/deade2.jpg  
  
Mizoga ya tembo waliouwawa na majangili
    
Simba akitafakari namna ya kuanza kula mzoga wa tembo
   
Tembo ni wanyama wenye akili sana na wanafundishika. Hapa ni mtunza wanyama hao akimbuzu tembo
     
Mtunza wanyama akikumbatiana kwa upendo na tembo
   
Mtunza wanyama akimnywesha maziwa mtoto wa tembo ambaye mama yake aliuwawa na maharamia
  
Hii ni shehena kubwa ya meno ya tembo iliyokamatwa na askari wa wanyama pori huko Kenya
 
Hii ni shehena ya meno ya tembo ambayo ilishafungwa tayari kusafirishwa China

 Wakati Jeshi la Polisi Jijini Arusha likiendelea kumhoji mtu aliyekamatwa na nyara nyingi za Serikali, nchini Kenya katika mbuga ya Tsavo mpakani na Tanzania familia nzima ya tembo 11 imeuwawa na kukatwa meno yake usiku wa kuamkia leo. Huu ni msiba mzito kwa  kenya kwani katika historia ya nchi hiyo haijapata kutokea kwamba tembo kumi na moja wameuwawa kwa wakati mmoja. Tembo wote 11 wamekutwa na majeraha makubwa ya risasi na meno yamekatwa.
Kuuwawa kwa tembo, faru na wanyama wengine ni kutokana na kushamiri sana kwa biashara ya meno ya tembo, pembe za faru huko Asia hasa Uchina. Kilo moja ya meno ya temba inauzwa dola nyingi sana na uhiitmeno hayo ni mkubwa mno kiasi  kla mtu anayepata upenyo  na asiye mzaledo, na aliye mbinafsi anafanya uhalifu wa kuwauwa wanyama hawa ilimradi tu atajirike haraka haraka.
Uuwaji huu umepelekea msako mkali unaoendelea sasa kujaribu kuwakamata majangili hao kwa kutumia askari wa miguu, kikosi cha mbwa na ndege.

May 2012 kontena lenye meno 359 na uzito wa tani moja na nusu lilikamatwa Sri Lanka na baada ya uchunguzi ilibainika kwamba zilitokea Kenya kupitia bandari ya Mombasa
Polisi pia  walikamata meno 214 yenye thamani ya dola moja 1.23 zilizokuwa zimefichwa kwenye majeneza na mifuko ya fertilizer zikiwa zimetokea Tanzania tayari kusafirishwa kupitia bandari ya mombasa kwenda china
Kwa hali ya uchumi ilivyo kwa wakenya na watanzania wengi, nafasi ikiatikana ya kujipatia fedha tena nyingi bila kodi, bila jasho basi sioni ni kwa namna gani tutaweza kuwalinda wanyama hawa wasiangamizwe. Ukifanya tathmini, hata askari wa wanyama pori wanaowalinda mishahara yao ni ya dhiki, hivyo ni rahisi kwao kutoa ushirikiano kwa maharamia au wenyewe kugeuka kuwa maharamia.
Nafikiri ili biashara hii ife, sisi tunaoathirika tungegomea bidhaa zote au ushirikiano na nchi ambamo  meno  haya na pembe hizi zinauzwa. Sisi tunatumia rasilimali nyingi kuwalinda wakati wenyewe wanatumia uwezo wao wa fedha kuzipata. Tutahangaika tu na wanyama wataendelea kuisha kidogo kidogo.
Kama tunauza wanyama hai tena kwa bei rahisi kabisa kwa wale ambao tunatarajia ndio wawe watalii kuna haja gani tena kwa mtalii kuja kupoteza pesa yake mbugani ilhali anaweza kuwaona pale pale kwao? Tusingekubali kuuza wanyama hai hata kidogo.
Ipo siku sisi ndio tutaenda kwao kuangalia wanyama. Urithi tutakaowaachia wajukuu zetu ni historia tu kwamba hapo kale kulikuwa na mbuga nyingi na nzuri zenye wanyama wa kila aina, lakini walikuja watu weupe na pesa zao wakawanunua tena kwa hela ya chumvi na kuwapeleka kwao wote na sasa hatuna tena hata mmoja, hivyo ukitaka kuwaona ni lazima upande ndege uende marekani, uarabuni, ulaya ukawaone. Huo ndio urithi wetu


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...