ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, January 9, 2013

Ndejembi: Shellukindo unamharibia Lowassa


 Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa 
Kwa ufupi
“Mimi sina shida na Lowassa, tena ni rafiki yangu na hata Kikwete sina shida naye. Kama upungufu, vijana hawa wanao kama binadamu wengine, lakini nakataa, hivi ni kwa nini
SharMWANASIASA mkongwe nchini na Kada wa CCM, Pancras Ndejembi amejitosa kwenye mjadala wa mbio za urais mwaka 2015 kwa kuwaonya makada wa chama hicho wanaowaza sasa kwenda Ikulu, akisema hii ni hatari kwao na kwa chama.

Ndejembi alienda mbali na kuwaponda wanaojitokeza na kudai wanawaunga mkono baadhi ya watu kwenye uchaguzi huo akisema ‘hii siyo sawa’.Ndejembi ambaye amevuma katika medani za siasa ndani na nje ya nchi, alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Mtaa wa Uzunguni mkoani Dodoma.

“Mimi sina shida na Lowassa, tena ni rafiki yangu na hata Kikwete sina shida naye. Kama upungufu, vijana hawa wanao kama binadamu wengine, lakini nakataa, hivi ni kwa nini tuanze suala la urais sasa,” alisema na kuongeza:

“Jambo hilo ni hatari, tena hatari kubwa ndani ya chama. Tutakuwa vipande na hata hao wagombea watarajiwa wenyewe tunawaongezea maadui bure bila sababu.”
Mkongwe huyo wa CCM alienda mbali zaidi na kumtaja Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shellukindo kwamba amekosea kujitokeza sasa kwamba atamuunga mkono Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa mwaka 2015.

“Huku ni kuacha maadili ya chama na kutoka nje ya mstari. Ni hatari kwake na kwa anayemfanyia kampeni hizo. Pia ni kinyume na kanuni za CCM.” alisema Ndejembi.
Ndejembi alieleza kuwa Shellukindo hakupaswa kujionyesha hadharani sasa kwamba anamuunga mkono Lowassa kwani huu ni wakati wa kutekeleza sera na Ilani ya uchaguzi ya chama.

Alisema kuwa kitendo cha kutamka hadharani kina athari pande zote ikiwamo ndani ya chama na hata kwa mgombea mwenyewe kwani anaongezewa maadui.

Aliwataka wanachama wa CCM hasa wabunge kuwa makini na kauli zao ili kutotumia vibaya fursa ya kuwa wawakilishi wa wananchi kwa kutaka wanaowaongoza wafuate matakwa yao.Akitumia nukuu za Marehemu baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Ndejembi alisema kuwa si dhambi kwa mtu kuonesha nia ili watu waanze kumpima, lakini kosa linakuja pale ambapo kiongozi ambaye ni mwakilishi wa wananchi anaposimama na kuanza kutoa kauli nzito za kumuunga mkono mtu anayemtaka.

“Kama nilivyosema, sina ugomvi na Lowassa, sina kabisa. Tunatofautiana kwa mambo machache sana ambayo ni ya kawaida kwenye siasa,” alisema Ndejembi.

Alipoulizwa kama yeye atamuunga mkono nani katika mbio hizo za urais, Ndejembi alijibu, “Nitasema wakati ukifika.”Januari Mosi, mwaka huu Shellukindo alieleza kuwa atafanya uamuzi mgumu mwaka 2015 ili kuhakikisha Lowassa anakuwa mrithi wa Rais Kikwete mwaka 2015.

Alisema chaguo lake kwenye uchaguzi huo ni kwa mtu mwenye uwezo wa kufanya uamuzi mgumu, kwa wakati na mzalendo kwa nchi yake.

Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...