Rais Obama akiapa huku Mke wake akishika Biblia na huku watoto wake Malia na Sasha wakimtazama kwa makini
Mama Obama akimwangalia Mumewe kwa namna ya kupendeza
Jaji aliyemwapisha Obama akimpongeza baada ya zoezi hilo kukamilika
Mwanaye wa Kwanza Malia (Mrefu kama baba na mama) akimkumbatia mzee huku Sasha naye akijiandaa
Wenye wivuuuuuuu...!
Umati uliokusanyika katika Ukulu wa White House ingawa hawakuwa wengi kama wale wa kipindi cha kwanza
Bibi yake Obama pia alikuwa anafuatilia kwa karibu
Ukulu wa white house ulivyokuwa umepambwa kwa bendera za Marekani (Hapa kwetu zingetawala bendera za chadema/ccm/cuf-katiba mpya ifute mabendera kibaaaao)
Watumbuizaji
Watu walijawa na shangwe
Mzee mwenyewe akitoa speech fupi (nitaiweka video yake hapa punde)
Mwonekano kutokea dirishani
Baadaye kama kawaida yake wakajirusha kwenye viwanja mbalimbali
Mambo ya wapendanao kwa dhati hayo
Wametokezea kweli kweli
Wakiaga na mwenda viwanja vingine walikokuwa wanasubiriwa
Mama na wattoto fasta wameshabadilisha mwonekano
Watu wamafurahi sana
At last (love and support is always very crucial)
RAIS Barack Obama wa Marekani ameapishwa rasmi kushika muhula wa
pili wa urais, katika sherehe maalumu iliyofanyika kwenye Ikulu ya nchi
hiyo jana.
Obama ambaye ni Rais wa 44 wa Marekani, aliingia
madarakani katika uchaguzi wa kihistoria mwaka 2008 uliomfanya kuwa Rais
wa kwanza mwenye asili ya Afrika katika taifa hilo kubwa duniani.
Sherehe za kuapishwa kwake Ikulu jana zilikuwa za
faragha na zilihudhuriwa na watu wachache maalumu, leo ataapishwa katika
sherehe za jumla zitakazowajumuisha watu wote kwenye Uwanja wa National
Mall.
Katika kiapo chake, Obama atatumia Biblia mbili,
moja iliyokuwa ikitumiwa na Martin Luther King na nyingine ilikuwa
ikitumiwa na aliyekuwa Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln.
Lincoln aliongoza taifa hilo kuanzia Machi 1861 hadi alipouawa Aprili 1865.
Akiwa Ikulu jana, alitumia Biblia iliyowahi kutumiwa na Lincoln, katika sherehe za leo atatumia Biblia ya Martin Luther King.
Lincoln, ndiye aliyeliongoza taifa hilo kipindi kigumu cha kusimamia umoja na kufuta biashara ya utumwa.
Lincoln aliongoza taifa hilo kuanzia Machi 1861 hadi alipouawa Aprili 1865.
Akiwa Ikulu jana, alitumia Biblia iliyowahi kutumiwa na Lincoln, katika sherehe za leo atatumia Biblia ya Martin Luther King.
Lincoln, ndiye aliyeliongoza taifa hilo kipindi kigumu cha kusimamia umoja na kufuta biashara ya utumwa.
Martin Luther King ambaye alikuwa mchungaji na
mwanaharakati wa haki za watu wenye asili ya Afrika nchini Marekani,
aliuawa Aprili 4, 1968, muda mfupi baada ya kutoa hotuba yenye nguvu ya I
have a Dream (Nimeota ndoto).
Hotuba hiyo ikuwa ikieleza ndoto yake kwamba muda
siyo mrefu watu wenye asili ya Afrika watapata nguvu na kupata haki yao
kama raia wa Marekani.
Viongozi hao wawili wana historia ya pekee,
Lincoln ndiye aliyetumia muda wake mwingi akiwa Ikulu ya Marekani
kuhakikisha watu wenye asili ya Afrika ambao walikuwa watumwa
wananasuliwa utumwani.
Luther alikuwa mwanaharakati aliyechochea mabadiliko kwa kushinikiza Serikali kuwapa haki zao za msingi.
Obama aliapishwa rasmi jana ikiwa ni siku ya
kwanza kati ya siku mbili zilizopangwa, leo ataapishwa mara ya pili
katika viwanja maalumu vya Nationa Mall mjini Washington, ambako maelfu
ya watu watapata fursa ya kushuhudia.
Hotuba ya kuapishwa kwake itakayotolewa leo
inatarajiwa kuweka historia mpya, pia kuhitimisha matukio ya siku mbili
hizi za kuapishwa, ataweka wazi mtazamo wake wa kipindi cha miaka minne
ijayo.
Mkusanyiko utakaoshuhudia kuapishwa kwake na
kusikiliza hotuba yake moja kwa moja katika uwanja huo unakadiriwa
kupungua kutoka ule wa watu 1.8 milioni mwaka 2009 na kufikia kati ya
600,000 na 800,000, huku mamilioni wakishuhudia kupitia televisheni.
No comments:
Post a Comment