Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili leo Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kupokelewa na Kaimu Balozi wa Tanzania
nchini humo Bwana Hemed Mgaza (katikati) Kushoto ni Mwenyekiti wa Bunge
na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (Mb). Kulia ni Mhe. Sadifa Juma Khamis,
(Mb).Mhe. Spika ameongoza ujumbe wa Wabunge watano kuhudhuria Mkutano wa
tatu wa Kimataifa wa Jukwaa la Kibunge la nchi za Ukanda wa Maziwa
Makuu.
Jukwaa
la Mabunge ya Jumuiya ya Kimataifa ya nchi za Ukanda wa Maziwa Mkuu
(FP-ICGLR) limeitaja Tanzania kuwa mfano wa kuigwa kwa juhudi
inazozifanya kuleta amani barani Afrika.
Pongeli
hizo zimetolewa leo na jumla ya nchi wa kumi na mbili zinazounda Jukwaa
hilo kwenye mkutano wa tatu unaoendelea kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC) zimewataja Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya
Mrisho Kikwete pamoa na watanzania kama wapenda amani barani Afrika.
Hii
ni kutokana na viongozi hao kujitolea kusuluhisha migogoro ya
DRC/Rwanda na kundi la M23, migogoro ya Afrika ya Kati, mgogoro wa
Sudani na Sudani Kusini, mgogoro wa Kenya baada ya uchaguzi mkuu na
mingine mingi. Pamoja na Tanzania, Afrika Kusini nayo imepongezwa.
Bunge
la Tanzania limewakilishwa na Spika wa Bunge ambaye ameongoza ujumbe wa
wabunge watano ambao ni Mhe. Mussa Azzan Zunge, Mhe. Pauline Gekul, na
Mhe Sadifa Juma. Wengine ni Mhe. Mohamed Mbarouk na Mhe. Prudenciana
Kikwembe.
Spika Makinda na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende (kulia) wakiingia kwanye mkutano huo.
Ufunguzi
wa mkutano wa Tatu wa PF –ICGLR (Forum of Parliaments of International
Conference on Great Lakes Region – FP/ICGLR) mjini Kinshasa.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja ya maspika, Sekretarieti pamoja washirika wa maendeleo wa FP-ICGLR.(Picha na Prosper Minja-Bunge).
No comments:
Post a Comment