Serikali
ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Baraza la Sanaa la Taifa,
limebariki kufanyika kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania
2012/13 baada ya kuridhishwa na maandalizi yaliyo fanywa na Miss Tourism
Tanzania Organisation waandaaji wenye dhima ya kikomo ya kuandaa na
kuendesha mashindano hayo kitaifa na kimataifa, pia kwa kuzingatia
sheria za nchi, kanuni na Taratibu za mashindano.
Serikali
pia imeridhishwa na jinsi Fainali za ngazi za mikoa na kanda
zilivyofanyika kwa mafanikio,ambapo kila mkoa umepata washindi wenye
sifa za kuwakilisha mkoa husika katika Fainali za Taifa mwaka huu,ambapo
jumla ya warembo 60 waingia rasmi kambini leo katika hoteli ya
Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, kuanza mbio za kuwania Taji hilo la
Taifa.
Washindi
wa 1-5 wa Fainali za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano
mbalimbali ya Dunia yakiwemo ya International Miss Tourism World, Miss
Tourism United Nation, Miss Heritage World, Miss Tourism University
World, Miss Globe International n.k Miss Utalii Tanzania ,hadi sasa
tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss
Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism
World 2007-Africa, Miss Tourism Model Of The World 2008-Personality n.k
Fainali
za Taifa mwaka huu zimepangwa kufanyika wiki ya kwanza ya Februari
,wilaya ya Temeke na mkoa wa Dar es Salaam ukiwa umepewa heshima ya kuwa
wenyeji wa Fainali hizo.
No comments:
Post a Comment