Fatima Mwanamama anayejulikana kwa jina la Utani Guavara au Lady Syria akiwa katika kiota chake cha kudungulia askari wa Serikali ya Syria
Fatima ambaye ni mama wa watoto wawili, aliamua kuingia vitani baada ya watoto wake wawili kuuwawa na majeshi ya serikali ya syria huko Allepo
Mashine ya kisasa kabisa anayoitumia Guerava ambayo anasema imezaa matunda ya kutosha
Kiota chake cha kuwindia wanajeshi wa Serikali
Guevara akifurahi baada ya kulenga baadhi ya maadui zake
Hii ndiyo darubini ambayo huwa anaiangalia kwa makini kwa jicho moja wakati mwingine kwa masaa matano kabla hajamlenga adui kazi ambayo anakiri si rahisi
Baada ya kudungua adui inabidi ahame haraka kwenye kiota hicho kwani maadui zake hujua kwamba pana kiota hivyo hutuma ndege na kupalipua
Guevara akishangilia baada ya kulenga maadui
Guevara akilenga shabaha
Haya ndiyo matukio yaliyomfanya Fatima kuuweka pembeni uanamke wake, dini yake na huruma yake kama mama na kuamua kuanza harakati zakijeshi
Fatma (Guevara) ni mwana dada wa kipekee katika ulimwengu wa Kiislam kwani si kawaida kwa akina mama kuingia vitani. Lakini machungu yaliyompata Fatima wakati watoto wake wawili walipouwawa na majeshi ya serikali na yeye mwenyewe kunusurika kifo, alimwomba mumewe ruhusa ya kulipiza kisasi lakini mumewe akikataa. Fatma aliachana na mwanaume huyo na kuolewa na kamara mkuu wa kikosi cha waasi cha Allepo ndipo alipofundishwa kushika bunduki ya kisasa na kupewa jukumu la kukaa kwenye viota (snipper) na kudungua maadui kwa mashine zisizokuwa na mlio.
Hata hivyo Fatma ambaye kwa sasa anajulikana kama Lady Syria au Guevara ameonyesha ukakamavu wa hali ya juu sana hata kuwashinda wanaume wengine. Sio tu anakaa katika viota bali pia anakuwa mstari wa mbele katika mapambano. Guevara ameshuhudia wanajeshi wenzake (comrades) zaidi ya mia moja wakiuwawa na hii imemfanya kutokuogopa kufa. Ameshaponea chupuchupu mara nyingi na anaamini kuw wakati wowote atauwawa, na hii ndiyo inayompa morali kwa kuwa hana cha kupoteza tena baada ya watoto wake kuuwawa.
Syria inazidi kuingia katika mgogoro mkubwa wa kibinadamu kwani sasa watu wanauwawa kama kumbikumbi na haijulikani ni lini mauwaji yataisha. Waathiriak wakubwa wa vita hivi ni akina mama na watoto.
No comments:
Post a Comment