Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
(Pichani) amewataka wakatoliki na watanzania kwa jumla kuwa watulivu
katika kipindi hiki ambapo kumetokea kundi la watu wachache kutaka
kuvunja amani hapa nchini kwa kutumia udini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kardinali Pengo
amesema moyo wa kisasi hautasaidia kitu chochote, kinyume chake utaleta
maafa yaliyo makubwa zaidi na kutuingiza katika janga kubwa zaidi.
Ameongeza
kuwa siku ya tarehe 20 kutakuwa na ibada katika Kanisa Kuu la Mtakatifu
Joseph itakayoongozwa na Askofu Msaidizi kwa lengo la kumuombea
marehemu Padri Evarist Mushi na kuliombea taifa ili watanzania tuendelee
kuwa wamoja na tubaki katika amani tuliokwisha kuizoea.
Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo amezungumza hayo baada ya kusoma waraka
uliotolewa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu uliozungumzia
mambo mengi ikiwemo kuwataja wakatoliki kama ‘makafiri’ na kuwa bado
haijawa mwisho wa mapambano.
No comments:
Post a Comment