Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na
Mchungaji Trafaina Aseri Nkya ambaye pia ni msaidizi wa Askofu Mteule
wa Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria na ujumbe wake
walipofika nyumbani kwake eneo la Ngarashi kijijini kwake Monduli,
kumshukuru kwa harambee ya ujenzi wa kanisa lao aliyoiendesha Januari
mwaka jana na kupatikana kiasi cha shilingi millioni 200 zikiwa ni fedha
tasilimu pamoja na ahadi.
ujumbe wa kamati ya ujenzi wa kanisa hilo ukimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasindiki zawajumbe hao.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,
amewataka vingozi wa dini nchini, kusaidia na kurejesha hali ya amani
kati ya wasilam na wakiristo ambayo inaonekana inaanza kupotea.
Akizungumza
hayo nyumbani kwake Monduli, wakati alipokuwa akipokea ujumbe kutoka
kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa
amesema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buserere, yanasikitisha sana
na kuongeza kuwa ni dalili mbaya ya kutoweka kwa amani ya Tanzania.
``Rais
ameelezea masikitiko yake, kwa kweli inasikitisha sana, mimi nawaomba
viongozi wa dini na madhehubu yote wasimamie na kuzuia mambo haya,
nawaomba watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu
isipotee`` alisema Lowassa kwa masikitikiko makubwa.
Katika
fujo hizo za Buserere,mchungaji mmoja wa kanisa la sabato aliuwawa
baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya waislam na wakristo.Chanzo cha
mapigano hayo kilikuwa ni wakristo kuamua kuchinja ng'ombe na kuuza
kwenye bucha lao, hatua iliyopingwa na wananchi wa dini ya kiislam
kwenye eneo hilo.
No comments:
Post a Comment