Picha na NYDailynews.com
Serikali
ya Venezuela imetoa hadharini kwa mara ya kwanza picha za rais Hugo
Chaves ambae hajaonekana katika macho ya umma wa taifa hilo tangu
Desemba mwaka jana.
Katika
picha hizo rais Chaves anaonekana amelala kitandani huku Mabinti wake
wawili wanaonekana wakiwa wamesimama pembezoni mwake.
Kiongozi
huyo mwenye umri wa miaka 58 anaendelea kurejea katika afya yake baada
ya kupata matatizo yanayohusishwa na upasuaji wa ugonjwa wa saratani.
Mpaka
sasa serikali ya Venezuela anaendelea kumsubiri Chaves apate nafuu ili
aweze kuapishwa ili kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine wa miaka
sita.
No comments:
Post a Comment