Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati)
akifuatana na Askofu wa Kanisa
Katoliki Jimbo la Zanzibar Augustino Shao wakielekea katika Mazishi ya Padri Evaristus Gabriel
Mushi,aliyezikwa katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja
|
Askofu
Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga Antony Banzi,akiongoza sala wakati wa mazishi ya Marehemu
Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyekufa kwa kupigwa risasi Jumapili Iliyopita na kuzikwa leo katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya kaskazini B Unguja jana
Vijana
waumini
wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha jeneza lenye mwili wa marehemu Padri
Evaristus Gabriel Mushi,katika kaburi alilozikwa jana katika viwanja
vya kanisa la Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu
alifariki kwa kupigwa risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.
Askofu
wa Kanisa Katoliki Jimbo la
Zanzibar Augustino Shao, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri
Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa jana katika viwanja vya kanisa
Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Rais
wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein,(katikati)
akitia udongo katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake
yaliyofanyika jana katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini
B Unguja.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emanuel Nchimbi ,akitia udongo
katika kaburi la Marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa
mazishi yake yaliyofanyika jana katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja
Vijana
waumini wa Dini ya Kikiristo wakiteremsha udongo wakati wa mazishi ya marehemu Padri Evaristus Gabriel Mushi,katika
kaburi alilozikwa jana katika viwanja vya kanisa la Katoliki la
Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,marehemu alifariki kwa kupigwa
risasi Jumapili iliyopita na watu wasiojulikanwa.
ASkofu
Mkuu
wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadham Policup Kadinari Pengo,kwa pamoja
na maaskofu wengine wakichomeka Msalaba katika kaburi la marehemu
Padri Evaristus Gabriel Mushi,aliyezikwa jana katika viwanja vya kanisa
Katoliki la Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,ambae alifariki
Jumapili Iliyopita kwa kupigwa risasi na watu wasiojukanwa.
Rais
wa Zanbzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed
Shein,(katikati) akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Padri
Evaristus Gabriel Mushi,wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika viwanja vya kanisa la Kitope,Wilaya
ya Kaskazini B Unguja.
Baadhi ya waumini wa kanisa katoliki
wakiwa katika mazishi ya marehemu Padri Evaristus Gabriel
Mushi,aliyezikwa jana katika viwanja vya kanisa Katoliki la
Kitope,Wilaya ya Kaskazini B Unguja,Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar
---
Na Maelezo Zanzibar
Mamia ya Wananchi wa Zanzibar jana
wameshiriki Mazishi ya Padri Evaristus Mushi aliyeuwa kwa kupigwa Risasi na
Watu wasiojulikana ambayo yamefanyika katika kijiji cha Kitope Wilaya ya
Kaskazini B,Unguja.Katika mazishi hayo Rais wa Zanzibar
Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff
Hamad,Viongozi wa Serikali na Vyama vya siasa walihudhuria.
Akitoa salamu za Serikali katika Mazishi
hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed
alisema Serikali imeguswa sana na kifo cha Padri huyo na kuongeza kuwa
itahakikisha waliohusika na tukio la mauji hayo wanakamatwa na kufikishwa
katika vyombo vya sheria.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Anglikacana
Michael hafidh amewataka Waamini wa dini ya kikristo kuwa watulivu bila
kulipiza kisasi bali waiachie Serikali kufanya kazi yake ili kuwabaini
waliopoteza Uhai wa Marehemu huyo.
Awali Mazishi hayo yalitanguliwa na Misa
takatifu ya kumuombea Marehemu iliyoendeshwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki
Jimbo kuu la Dar es Salaam Muadhama Policarp Kadinali Pengo katika Kanisa la
Minara Miwili Mjini Zanzibar.
Padri Mushi alifariki dunia Februari 17 baada
ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akielekea Kanisani kuendesha
Misa ya Asubuhi katika Kigango cha Mtakatifu Teresia eneo la Beit El Raas
mjini Unguja Enzi za uhai wake Padri Mushi alikuwa Msomi wa Shahada ya Uzamivu
ya Elimu ya Ushauri nasaha aliyoipata nchini Marekani ambapo umauti ulimkuta
akiwa anaelekea kuendesha Ibada ya Jumapili ya kwanza ya Kwarezma.
Padri Evarist Mushi wa Kanisa la Minara Miwili
mjini Zanzibar alizaliwa June 15, 1957 Mkoa wa Kilimanjaro akiwa ni mtoto wa
nne katika familia ya watoto sita ya Mzee Mushi.
No comments:
Post a Comment