SERIKALI ya Zimbabwe imesema kwamba mpaka sasa kiasi cha fedha ambacho kipo kwenye akaunti ya Serikali ni Dola 217.
Kiasi
hicho ambacho ndicho kinachotajwa kulinda akaunti hiyo ya Serikali ni
sawa na Sh347 za Tanzania, huku nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mkuu
miezi michache ijayo.
Akizungumza jana nchini humo, Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Tendai Biti alisema kwamba kiasi hicho cha fedha ndicho kilichobaki katika akaunti hiyo baada ya kuwalipa wafanyakazi wake mishahara wiki iliyopita.
Biti alisema kwamba kwa sasa Serikali ya nchi hiyo inakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kutokuwepo fedha katika akaunti ya Serikali huku vyanzo vingi vya mapato vikiwa bado havina uhakika.
Kwa mujibu wa Biti ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change, MDC alisema kwamba kutokana na hali hiyo, Rais Robert Mugabe amemwagiza kuanza kuwasiliana na wafadhili kwa ajili ya kupata misaada kutoka nje.
Mataifa mengi wafadhili hasa yale ya Magharibi, yameipa kisogo Zimbabwe kwa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi vinavyowalenga zaidi washirika wa Rais Robert Mugabe na Chama cha Zanu-PF.
No comments:
Post a Comment