Oscar Pistorius alizaliwa mlemavu wa miguu lakini ulemavu wake haukumzuia kufikia ndoto zake.
Oscar Pistorius akiwa anafanya mazoezi
Mwanariadha Oscar Pistorius alipokuwa katika mashindano ya Olympic mwaka 2012 mjini London.
Mwanariadha na mshindi wa medali za dhahabu wa Paralympic raia wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, amekamatwa nyumbani
kwake mjini Pretoria kwa kosa la kumuua mpenzi wake baada ya kumpiga
risasi moja kichwani na nyingine mkononi , majeraha yaliyopelekea kifo
cha binti huyo.
Chanzo
cha Pistorius kumsuti mpenzi wake bado hakijaeleweka, japo fununu za
awali zinadai uenda Pistorius alijichanganya na kudhani amevamiwa na
mwizi/jambazi kutokana na hali mbaya ya uhalifu anayoikabili nchi ya
Afrika Kusini.
Binti huyo Reeva Steenkamp, (30) mwanamitindo alilenga kumsuprise Pistorius kwaajili ya valentine.
Msemaji
wa Polisi aliliambia shirika la habari la Reuters “tumekuta pisto ya
mm9 eneo la tukio, na mtuhumiwa amepelekwa kituoni kwaajili ya utaratibu
mwingine”.
Pistorius
mwenye miaka 26 maarufu kama “blade runner” amekuwa ni mlemavu wa
kwanza kushiriki Olympic mbali na mashindano yao maalum ya Paralympic ,
hukimbia riadha kwa kutumia vifaa maalum vilivyofungwa miguuni kwake, baada ya kuzaliwa bila miguu yote miwili.
No comments:
Post a Comment