Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema akitoa taarifa ya jeshi hilo mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi hilo leo mchana.
Nimelazimika
nizungumze nanyi kuhusu tukio la kuuwawa kwa Padre Evaristi Mushi wa
Kanisa Katoliki Zanzibar lililotokea leo asubuhi tarehe 17 Februari,
2013 eneo la Mtoni mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo watu wasiofahamika
walimpiga risasi Padre huyo alipokuwa anaenda kusalisha ibada katika
kanisa la Betras. Baada ya tukio hilo kutokea alikimbizwa katika
hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo baadae alifariki dunia. Tukio hili ni
baya na la kusikitisha.
2 Kufuatia kutokea kwa tukio hilo na kujirudiarudia kwa vitendo vya
kuwashambulia na kuwadhuru viongozi wa dini na uchomaji wa nyumba za
ibada, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na
usalama tumeanza uchunguzi wa kina wa kuwatafuta wanaohusika na
matukio hayo.
3Hivyo, nimetuma timu ya wataalam waliobobea kwenye masuala ya
upelelezi na oparesheni kutoka Makao Makuu ya Polisi, kwenda
kushirikiana na timu ya wataalam iliyoko Zanzibar. Hadi sasa watu
watatu wananshikiliwa kwa mahojiano.
Jeshi la Polisi limeimarisha doria maeneo yote hapa nchini na
tunafuatilia mienendo na kuakamata watu wote wanaochochea, kufadhili,
kuhamasisha na kushiriki katika vitendo vya uhalifu, vurugu na fujo.
Tukiwa katika kipindi hiki, nawaomba wananchi wote hapa nchini kuwa
watulivu wakati suala hili linaposhughulikiwa kuhakikisha kwamba
wahalifu hao wanakamatwa na sheria inachukua mkondo wake.
Naomba nitumie fursa hii pia, kuwasiliana na wananchi wenzangu wenye
taarifa zitakazosaidia wahalifu hao kukamatwa kutupa ushirikiano
kupitia namba zetu maalum za simu zifuatazo 0754785557 au 0782417247 na
namba za makamanda wa mikoa na vikosi, ili kuhakikisha kwamba amani,
usalama na utulivu vinadumishwa hapa nchini.
Nawashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakitupa ushirikiano.
AHSANTENI SANA.
No comments:
Post a Comment