WATU watano wamepoteza maisha na
wengine 130 wamejuruhiwa vibaya huku hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori
walilokuwa wakisafiria shambani kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha
Mapogolo kata ya Itamboleo Wilayani Mbarali Mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30
asubuhi ambapo lori hilo ambalo ni mali ya Mwekezaji wa shamba la Kapunga
Rice Project, na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye shamba la mwekezaji
huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha
Kapunga.
Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika hospitalini hapo alisema
kuwa mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya
,Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa kuongezewa
madaktari, kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na uwezekano wa kupata damu
kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa
hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya kwenda
kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro, alisema kuwa
katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na mwanamke mmoja. watatu wametambuliwa
Samweli Mapugilo mbena 30 mkazi wa Ilembula
Bon Mfupa 27 mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde Mbeya
No comments:
Post a Comment