Jeshi la Korea
Kaskazini leo limekata mawasiliano ya simu na Korea Kusini, na kusitisha
mawasiliano ya mwisho ya moja kwa moja baina ya nchi hizo mbili, katika
wakati
ambapo kuna hofu kubwa ya kijeshi.
Hatua hiyo imechukuliwa sambamba na
tangazo kwamba viongozi wakuu wa kisiasa wa Korea Kaskazini watakutana
katika siku chache zijazo kujadili kuhusu "suala muhimu" na kufanya
uamuzi wa kurudi nyuma. Hatua ya kukata mawasiliano ya simu imetangazwa
na afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la Kaskazini kwa mwenzake wa kusini
muda mfupi kabla ya kukatwa laini hizo za simu. Wiki chache zilizopita,
Korea Kaskazini ilikata laini za simu za Shirika la Msalaba Mwekundu
ambazo zilikuwa zimetumiwa katika mawasiliano ya kiserikali bila kuwepo
uhusiano wa kidiplomasia. Hatua hiyo ya kukatwa mawasiliano ya simu
ndiyo ya karibuni katika msururu wa vitisho na hatua kutoka serikali ya
Pyongyang na kuongeza hofu katika Rasi ya Korea tangu uzinduzi wa Korea
Kaskazini wa kombora la masafa marefu mwezi Desemba na majaribio yake ya
nyuklia mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment