
Mmoja wa wale waliojeruhiwa
Taarifa ambazo bado
hazijathibitishwa zinasema kuwa watu 10, wakiwemo maafisa wa polisi
wawili, wameuawa mjini Mombasa, Pwani ya Kenya. Tukio hilo lilitokea
alfajiri, kuamkia leo wakenya wanapopiga kura.
Hata hivyo polisi walithibitisha vifo vya
maafisa wao wawili vilivyotokea wakati polisi walipowapiga risasi
washambulizi waliokuwa wamejihami kwa mapanga. Lilikuwa shambulizi la
kulipiza kisasi.Washambulizi hao wanashukiwa kuwa wafuasi wa kundi la Pwani la Mombasa Republican Army (MRC) ambao wamekuwa wakipigania uhuru wa jimbo la Pwani.
Mwandishi wa BBC, Karen Allen, anasema polisi waliweza kuthibitisha vifo vya wanne katika eneo la Changamwe, naye Hassan Majid aliona mtu mmoja kauawa eneo la Mishomoroni. Mwtu mwingine Moja ya miili hiyo ilikuwa imekatwakatwa.
Zaidi ya watu 1,000 waliuawa miaka mitano iliyopita katika ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment