Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwasili katika Shule ya Msingi
Kigilagila iliyopo maeneo ya Gongo la Mboto kama mgeni rasmi katika
hafla fupi iliyoandiliwa na mfuko wa Pensheni wa PPF ya kukabidhi vitabu
kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Mgeni
rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akitambulishwa kwa
Meneja wa Penesheni Bi. Chevu Sepeku( kushoto) mara baada ya kuwasili
katika shule hiyo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda
ya Ilala Bw. Evans Musiba na Wa pili kulia ni Afisa Uhusiano wa Pensheni
wa PPF Bi. Lulu Mengele.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiteta jambo na mmoja wa wanakikundi cha kwaya cha shule hiyo mara baada ya kuwasili.
Kwaya ya Shule ya Msingi Kigilagila ikipiga wimbo wa Taifa kuashiria kuanza kwa hafla hiyo.
Meza
kuu wakiupa heshima wimbo wa Taifa: Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry
Silaa (wa pili kushoto), Meneja wa Penesheni Bi. Chevu Sepeku( kulia) ,
Wa pili kulia ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans
Musiba na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kigilagila Verian
Mfugale.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Kigilagila Verian Mfugale akiukaribisha ugeni
katika shule hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi za vitabu
shuleni hapo pamoja na kwa watoto wawili yatima ambao wazazi wao
walikuwa ni wanachama wa mfuko wa Pensheni wa PPF na kuendelea
kusomeshwa kupitia FAO LA ELIMU linatolewa na mfuko wa Penesheni wa PFF.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza jambo na Meneja wa
Mfuko wa Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba wakati wa hafla fupi
ya kukabidhi vitabu iliyoenda sambamba na Kampeni ya Kutangaza FAO LA
ELIMU.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza na walimu na
wanafunzi wa shule ya Kigilagila na kufafanua kuwa mambo yanayofanywa na
Mfuko waPensheni wa PPF katika kurekebisha baadhi ya mafao yake haswa
fao la kifo, si tu yatasaidia kuwapa elimu wanafunzi wanaoguswa bali
yatatia mkono katika kuboresha elimu katika mfumo mzima wa taifa letu na
moja kwa moja katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.
Aidha
Mh. Silaa ametoa wito kwa watanzania akisema kwa kuwa sasa mifuko hii
ya pensheni imefungua milango, sio kwa watu walioajiriwa pekee ndio
wanaopaswa kujiunga na mifuko hii ya pensheni, lakini hata kwa watu
waliojiajiri, wakulima na hata wafugaji wana uwezo kabisa kisheria
kujiunga na mifuko ya pensheni na kunufaika nayo.
Pia
ameupongeza mfuko wa PPF kwa yale wanayoyafanya kwa watoto wa watu
waliofariki wakiwa wanachama wa mfuko huo, ambapo takwimu zinaonyesha
kuwa kwa mwaka 2012 jumla ya wanafunzi 1, 333 wamelipiwa gharama
mbalimbali zilizofikia jumla ya shilingi milioni 682.9 kitu ambacho ni
jambo la kupigiwa mfano.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba
akielezea nia ya kutembelea shule hiyo ni kutoa msaada wa vitabu kwa
sababu tunaamini kwamba vitabu tutakavyo vitoa vitawasaidia wanafunzi
waliopo hapa kuweza kupata elimu nzuri na kufanya vizuri katika mitihani
yao na vilevile hawa ndio viongozi wa baadae. Vilevile katika hii shule
ya Kigilagila sisi kama PPF tuna wanafunzi ambao tunawasomesha hivyo
sisi ni wadau wa shule hii na tunatumia fursa hii kuwashauri waalimu na
pia wazazi kujiunga na mfuko huu kwa manufaa ya baadae.
Meneja
wa Penesheni PPF Bi. Chevu Sepeku akitoa elimu kwa wageni na wanafunzi
waliohudhuria hafla hiyo kuhusiana na taratibu za utoaji wa mafao ya
Elimu na kufafanua kuwa hutolewa ili kugharamia sehemu au gharama zote
zinazohitajika katika elimu ya mtoto wa mwanachama aliyefariki ambapo
gharama hizo ni kuanzia elimu ya chekechea hadi kidato cha nne.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akikabidhi zawadi kwa mtoto wa darasa la Saba Ummy
Abdalah kwa niaba ya wanafunzi wenzake. Ummy Abdalah ni miongoni mwa
wanafunzi wanaosomeshwa na PPF kutumia FAO LA ELIMU baada ya wazazi
waliokuwa wananchama wa mfuko huu kufariki dunia.
Mtoto
Shakila Abdalah wa darasa la pili naye akipokea zawadi kutoka kwa
Mstahiki Meya Jerry Silaa. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Veriana
Mfugale akishihudia tukio hilo. Kwa picha zaidi bofya hapa
No comments:
Post a Comment