ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, March 14, 2013

Mwanamke mmoja huko Oklahoma ameshitakiwa kwa kujaribu kuwauza watoto wake ili apate fedha za kumuwekea thamana mchumba wake.

 

 



 
 
 
Polisi katika mji wa Wallisaw wamesema mwanamke huyo Misty VanHorn aliwasiliana na mnunuzi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Wamesema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa akitaka dola 1,000 kwa mtoto wake mwenye miaka miwili au dola 4,000 kwa mtoto wake mdogo mwenye miezi 10.
Anadaiwa kuandika katika face book akimuelekeza mnunuzi kuwa afike Sallisaw na atamkabidhi mtoto pamoja na vitu vyake vyote na kumuachia moja kwa moja.
Mwanamke huyo mnunuzi ambaye hajajulukana anayeishi jimbo la jirani la Arkansas alitoa taari kwa mamlaka za jimbo hilo.
Polisi walifika eneo hilo na kumkamata Misty VanHorn mara moja.
Majirani zake wamesema VanHom amekuwa akitembea mlango kwa mlango akijaribu kuchangisha dola 1,000 ili kumtoa mwenzi wake kwa dhamana.



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...