Jeshi
la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwaua majambazi saba wakati wa
mapambano makali ya kurushiana risasi na Askari wa Jeshi la Polisi
wakati majambazi hao walipokuwa katika harakati za kuvamia mgodi wa
Tulawaka ambapo baada ya kupekuliwa walikutwa na bunduki mbili za
kivita aina ya SMG, mabomu matatu ya kurusha kwa mkono, risasi 156,
magazine tano, simu mbili pamoja na fedha za Burundi franc 800.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Kamishna
Msaidizi wa Polisi Philip Kalagi alisema tukio hilo lilitokea tarehe
kumi mwezi huu majira ya saa tatu na nusu usiku katika kijiji cha Mavota
wilayani Biharamulo.
Kamanda Kalagi alisema kati ya majambazi hao, watano wanasadikiwa kuwa ni raia wa Burundi na mmoja wao ametambulika kwa jina la Minani Luzamba (46) mkazi wa Rwambarage nchini Burundi.
Aidha alisema raia wawili uraia wao bado unachunguzwa ingawa wamekutwa na vitambulisho vya Tanzania vya kupigia kura vilivyotolewa mkoani Kigoma na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Biharamulo.
Alisema kazi hiyo ilifanikiwa kwa kushirikiana na kikosi kazi cha taifa cha kuzuia uhalifu pamoja na taarifa za raia wema ambapo amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za kuwezesha kukamatwa kwa watu wanaojihusisha na uhalifu mkoani Kagera.
Aidha
Kamanda Kalagi alisema Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na msako
mkali kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
kuhakikisha mkoa huo unakuwa na usalama na wananchi wanafanya kazi zao
bila hofu ya uhalifu na wahalifu.Kamanda Kalagi alisema kati ya majambazi hao, watano wanasadikiwa kuwa ni raia wa Burundi na mmoja wao ametambulika kwa jina la Minani Luzamba (46) mkazi wa Rwambarage nchini Burundi.
Aidha alisema raia wawili uraia wao bado unachunguzwa ingawa wamekutwa na vitambulisho vya Tanzania vya kupigia kura vilivyotolewa mkoani Kigoma na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Biharamulo.
Alisema kazi hiyo ilifanikiwa kwa kushirikiana na kikosi kazi cha taifa cha kuzuia uhalifu pamoja na taarifa za raia wema ambapo amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za kuwezesha kukamatwa kwa watu wanaojihusisha na uhalifu mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment