ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, April 29, 2013

BODI YA MIKOPO YATANGAZA KUANZA KUPOKEA MAOMBI


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Bw. Cosmas Mwaisobwa akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam alipokua akitangaza kuhusu kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuanzia 1 Mei, 2013.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetangaza kuanza kupokea maombi ya mikopo kwa wafunzi wanaotarajiwa kujiunga na Vyuo Vikuu pamoja na wanafunzi wanaoendelea kwa mwaka wa masomo 2013/2014 kuanzia Mei 1, 2013.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Bodi hiyo Bw. Cosmas Mwaisobwa amewaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa maombi ya mikopo yatafanyika kwa njia ya mtandao kupitia anuani ya http://olas.heslb.go.tz.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...