Kikosi
cha kutuliza ghasia mkoani Arusha kililazimika kutumia Mabomu ya
Machozi kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wakishinikiza kuandamana baada ya
mwanafunzi mwenzao kuuawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana
majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo.
Tukio hilo liliamsha hisia za
wanafunzi hao na kuwafanya wakusanyike kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa
Arusha kwa madai kwamba matatizo yao huwa hayafikishwi ipasavyo, hivyo
wanataka kuyawasilisha wenyewe.
Juhudi za uongozi wa chuo kuwatuliza
wanafunzi hao zilishindikana, na ilipofika majira ya saa nne asubuhi,
Mbunge wa jimbo la Arusha alifika katika eneo hilo kuwasikiliza
wanafunzi hao.
"Tunatoa dakika thelathini mkuu wa mkoa awe ameshafika
hapa, kama hajafika ndani ya muda huo, tunaandamana wote, mimi mbele
nyie nyuma mpaka ofisini kwake" alisema
Mheshimiwa Lema.Baada
ya mkuu wa mkoa kufika eneo la tukio aligoma kuzungumza na wanafunzi
hao, akidai kwamba hawezi kuongea mpaka Mh.Lema aondoke, ndipo atapanda
kuzungumza na pia alilalamika kwamba hamna kipaza sauti kwa hiyo hawez
kupaza sauti yake kuzungumza na watu wasio na nidhamu.
Maneno hayo
yalipandisha hasira ya wanafunzi hao lakini walitulizwa, na kipaza sauti
kikaandaliwa katika ukumbi wa chuo maaruf kama "main cafetaria" ili
mkuu huyo azungumze.
Wanafunzi
walikusanyika eneo hilo kumsikiliza lakini alivyoanza kuongea,
wanafunzi walisikika wakimzomea kwa madai kwamba ameonesha dharau.
Wanafunzi walianza kuzomea na kumrushia chupa zaa maji na mawe mkuu wa mkoa na
hapo ndipo ilibidi mabomu ya machozi yatumike kuwatuliza wanafunzi wa
chuo hicho.
Kwa muda wa masaa mawili imekuwa ikisikika milio ya mabomu
chuoni hapo mpaka hali ilipo tulia kabisa.
Kwa
sasa hali ni shwari chuoni hapo ila polisi wametapakaa huku na kule
wakisema wanamtafuta Mbunge wa jimbo la Arusha kwa madai kuwa ndiye
anaye chochea mgomo huo wa wanafunzi.
Mbunge huyo alikimbia kuelekea kusikojulikana na kutelekeza gari yake chuoni hapo, ambayo polisi walilazimika kuivuta kwa "breakdown" car kuelekea kituo cha polisi. kama inavyoonekana katika picha.
Gari ya Mh.Godbless Lema ikiochukuliwa na polisi kutoka eneo la tukio
Polisi wakichukua gari ya mbunge wa jimbo la Arusha
No comments:
Post a Comment