Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar naKatibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi
akiwahutubia wananchi wa Mkwajuni katika mkuto wa hadhara wa chama hicho
uliofanyaka katika viwanja vya mpira Mkwajuni, April 06/2013
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi
akiwahutubia wananchi wa Mkwajuni katika mkuto wa hadhara wa chama hicho
uliofanyaka katika viwanja vya mpira Mkwajuni, April 06/2013
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi
akisikiza utenzi kwa makini,kulia ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Hamad
Masoud Hamad na kushoto Mwenyekiti wa Wilaya ya Kaskazini (A). huko
Mkwajuni Kaskazini A Unguja.
Wanachama wa CUF wakisikiliza kwa makini Maalim Seif Sharif Hamadi
hayupo pichani alipokuwa akiwahutubi katika mkutano wa hazara
uliofanyika katika viwanja vya mpira Mkwajuni.
--
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na katibu Mkuu wa Chama cha
Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar ni nchi ya
biashara hivyo inataka kujitegemea iweze kupunguza ushuru ili wananchi
wapate kununua bidhaa kwa bei nafuu.
Kauli hiyo ameitoa huko katika viwanja
vya Skuli ya Mkwajuni Wilaya ya kaskazini “A” wakati alipokuwa
akizungumza na wananchi wa Mkoa huo.
Amesema iwapo Zanzibar itapata mamlaka yake kamili itaweza kuwa na bandari huru, ushuru na bei za bidha vitapungua.
“Zanzibar ni nchi ya biashara tunataka
tuwe na bandari huru ili tupate kuweka kodi ndogo na ushuru ukipungua
bei za bidhaa zitapungua”alieleza Maalim.
Aidha amesema kuwa wananchi wanataka
kuwepo kwa bandari na kupungua ushuru ili wapate kuweka bei wanazotaka
wenyewe na sio kuamuliwa na mtu mwengine.
Akizungumzia Muungano Maalim Seif amesema
wazanzibari waliowengi wanataka serikali ya mkataba iwe na mamlaka
kamili na isiingiliwe katika maamuzi yake.
“Haya ni matakwa ya wananchi wenyewe na sio matakwa ya CUF hili ni la wazanzibar wenyewe” alieleza Katibu huyo.
“Zanzibar ni nchi matakwa ya wazanzibari
yaheshimiwe yasiingiliwe na wengine kwani mamlaka na madaraka hayo ndiyo
yanayoweza kuyatatua matatizo ya wazanzibar” alifafanua Maalim Seif.
Hata hivyo Katibu huyo ameitaka Tume ya
kukusanya maoni ya Katiba kuhakikisha kwamba wajumbe waliochaguliwa
kuwakilisha kutoa maoni katika Katiba hiyo wamechaguliwa kihalali na sio
kupandikizwa.
IMETOLEWA NA
IDARA YA HABARI MAELEZO- ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment