Mkurugenzi
wa Idara ya Utalii , Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Bw. Ibrahim
Mussa (kushoto) akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii ya
China Bw. Zhu Shanzhong juu ya masuala mbalimbali ya uhusiano baina ya
nchi hizi mbili hususan katika sekta ya utalii wa Tanzania katika soko
la China.
Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kushoto) na Kaimu Mhifadhi wa Mamlaka ya
Ngorongoro Bruno Kawasange wakifuatilia mazungumzo hayo.
Balozi
wa Tanzania nchini China Philip Marmo (kulia) na Mbunge wa Ngorongoro
Mhe. Kaika Telele wakifuatilia mazungumzo baina ya serikali ya Tanzania
na China kuhusiana na sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki (kulia) na Mkurugenzi
Msaidizi wa Malikale John Kimaro wakifuatilia mazungumzo hayo kwa
umakini.
Viongozi wa Serikali ya China wakifuatilia majadiliano. (Picha zote na mdau Pascal Shelutete, TANAPA)
Mkurugenzi
wa Idara ya Utalii Ibrahimu Mussa (kushoto) akipokea zawadi maalum ya
stempu mbalimbali za China kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Wizara ya
Utalii nchini China Zhu Shanzhong mara baada ya kumalizika kwa
mazungumzo yao.
Mkurugenzi
wa Utalii Ibrahimu Mussa na Balozi Philip Marmo wakiwa na Makamu
Mwenyekiti wa Wizara ya Utalii ya China Bw. Zhu Shanzhong
…………………………………………….
Pascal Shelutete, Beijing
Matangazo
ya moja kwa moja ya Mzunguko wa Nyumbu wahamao katika Hifadhi ya
Serengeti katika Televisheni ya Taifa ya China yameongeza mwamko wa
wachina kutembelea Tanzania kama watalii. Haya yalisemwa jana na Makamu
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utalii ya China Zhu Shanzhong alipokutana na
ujumbe kutoka Tanzania jijini Beijing China.
Shanzhong
alisema kuwa Hifadhi ya Serengeti ambapo vipindi kadhaa vimesharushwa
tangu mwezi januari mwaka huu nchini China, inaendelea kupata umaarufu
mkubwa miongoni mwa wananchi wa China na kuelezea matarajio yake kuwa
matangazo haya yataweza kuongeza idadi ya watalii nchini katika muda
mfupi ujao.
Alisema
kuwa ziaraya hivi karibuni iliyofanywa na Rais wa Ji Xinping nchini
imeendelea kuitangaza Tanzania nchini China na kuongeza kuwa upekee wa
vivutio vya utalii ni mtaji mzuri unaopaswa kutumika vizuri kutangaza
utalii na hivyo kuongeza pato la taifa.
Mapema
Makamu Mwenyekiti huyo alieleza haja ya kuwepo kwa ushirikiano wa
karibu baina ya sekta za utalii kwa nchi hizi mbili na kutaka kuandaliwa
kwa rasimu ya Hati ya Makubaliano itakayobainisha maeneo muhimu ya
kushirikiana kwa kuwa na mipango thabiti ya muda mrefu na mfupi.
Katika
mkutano huo, Shanzhong aliomba ridhaa ya Tanzania kuridhia ombi la
China la kuanza kutumia kwa lugha ya kichina kuwa mojawapo ya lugha
rasmi zitakazotumika katika vikao vya Shirika la Umoja wa Mataifa la
Utalii. Alieleza kuwa nchi yake imepeleka ombi hilo makao makuu ya
shirika hilo ambayo yanahitaji kuungwa mkono na zaidi ya nusu ya nchi
wanachama wa shirika hilo.Ujumbe wa Tanzania unaoongozwa na Mkurugenzi
wa Idara ya Utalii Ibrahim Mussa uliahidi kuwa Tanzania itaunga mkono
ombi hilo kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa UNTWO mapema mwezi
Agosti mwaka huu nchini Zimbabwe na Zambia.







No comments:
Post a Comment