Baadhi ya Wajumbe kutoka Wizara ya Fedha wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao. Kutoka
kulia ni Kamishna wa Bajeti Bi. Monica Mwamunyange, Mhasibu Mkuu wa
Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda pamoja na Kamishna wa Sera Bw. Beda
Shallanda.
Wajumbe
wakisikiliza kwa makini hoja zilizotolewa na Gavana wa Benki Kuu hayumo
pichani, Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa
BOT Dr. Joseph Masawe, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar
Bi. Bihindi Nassor pamoja na Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Benno Ndulu akitoa maelekezo kwa wajumbe
kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa Kipupwe. Gavana alikuwa
mwenyekiti wa kikao hicho kwa niaba ya Waziri wa Fedha.
Kutoka
kushoto Mkuu wa Kitengo cha Sheria Bi Susan Mkapa pamoja na Kamishna wa
Fedha za Nje Bw. Said Magonya wa Wizara ya Fedha wakisikiliza kwa
makini katika kikao hicho pembeni ni Mchumi mwandamizi wa Wizara ya
Fedha Bw. Patric Pima.
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Harry Kitilya akitoa ufafanuzi katika kikao cha pamoja cha wajumbe kutoka Tanzania kilichofanyika katika ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC.
Kutoka
kushoto Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Fedha
Bi. Ingiahedi Mduma, Msaidizi wa Gavana Bw. Msafiri Nampesya pamoja na
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Suleiman Saleh
wakisikiliza jambo kwa makini kutoka kwa Afisa Mwambata anayeratibu
masuala ya Uchumi, Biashara, na Uwezeshaji ya Benki ya Dunia na IMF Bw.
Paul Mwafongo.
Mikutano ya kipupwe imeanza rasmi mjini
Washington DC kuanzia tarehe 15/4/2013 na kuhudhuriwa na nchi wanachama zaidi
ya 188. Waziri wa Fedha Mhe. Dkt Augustiao William Mgimwa ni Gavana mmoja wapo
katika mikutano hiyo na Nchi ya Tanzania ni mwanachama katika mikutano hii.
Kila kunapokuwa na mikutano ya kipupwe
maelfu ya wafanyakazi wa Serikali, waandishi wa habari, mashirika yasiyo ya
kiserikali, washiriki waalikwa kutoka sekta za elimu na binafsi, wanakutana
mjini Washington DC kwa mikutano hii ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shrika la
Fedha la kimataifa pamoja na kamati za kifedha, ambazo zinajadili maendeleo ya
kazi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa. Aidha pamoja na
mikutano hiyo kunakuwa na semina na majadiliano mbalimbali, mikutano ya
waandishi wa habari na matukio mbalimbali yanayohusu uchumi jumla , maendeleo
ya kimataifa na masoko ya kifedha ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment