
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akilakiwa na
uongozi wa Starkey alipowasili katika shule ya Buguruni Viziwi kuzindua
kambi ya Starkey itakayokuwa inatoa huduma ya uchunguzi, vifaa na
matibabu bure kwa wananchi wenye matatizo ya kusikia.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo na mmoja wa wauguzi katika kambi hiyo mara baada ya kuwasili.

Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akifanyiwa
uchunguzi wa tatizo la kutosikia wakati kuzindua kambi ya Starkey
itakayosaidia kutoa huduma na matibabu bure kwa wananchi wenye matatizo
ya kusikia iliyopo kwenye shule ya watoto wenye ulemavu wa kusikia
(Buguruni viziwi) jijini Dar.
Mstahiki
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa jana tarehe 16
April 2013 amezindua kambi ya Starkey ya kusaidia
wananchi wenye matatizo ya kusikia iliyofanyika katika shule ya watoto
wenye ulemavu wa kusikia (Buguruni viziwi), ambapo wenye magonjwa
watatibiwa na wenye kuhitaji vifaa vya kuongezea usikivu watatengenezewa
kulingana na size zao na watapewa bureee.
Mstahiki
Meya amepima na kwa kuwa ameonekana kutokuwa na tatizo amepata fursa ya
kutengenezewa "custom made earphones" wote wenye matatizo
mnakaribishwa. Huduma hii ni bureee...

Picha
juu na chini ni Mstahiki Meya Jerry Silaa akivishwa "Custom made
earphones" na mmoja wa madaktari bingwa katika kambi hiyo mara baada ya
kuzindua huduma hiyo atakayokuwa ikitolewa bure kwa wananchi wenye
matatizo ya kusikia.


Mstahiki Meya Jerry Silaa akimsalimia mmoja wa watoto waliofika kambini hapo kupatiwa huduma baada ya kuizindua.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya namna huduma hiyo itakavyokuwa ikitolewa kwa wagonjwa watakaofika kambini hapo.

No comments:
Post a Comment