Chumbani kwa marehemu Oysterbay
Polisi wa Oysterbay wakitoa faili lao la uchunguzi
Mwili ukiondolewa Aga Khan
Mwili ukiwasili makaburi ya Wahindi Makumbusho Dsm
Kichanja cha kuchomea kikiwa tayari
Store ya kuni za kuchomea
Watoto wa marehemu Jimmy & Loose wakimuaga baba yao
Mpenzi wake Caroline akimuaga mpenzi wake
Mwanaye Jimmy akisema "It's Over"
Wafanyakazi wa makampuni ya kuchimba na kufanya utafiti wa mafuta na gesi
wa Swala Oil and Gas na Petrodel ambako alikuwa akifanya kazi wakimuaga
Wataalamu wa kuchoma miili wakijiandaa kuweka mwili
kwenye sehemu ya kuchomea
Farewell Dr. Philip Nelson
Mpenzi wake akipewa nafasi ya mwisho ya kumuaga rafiki yake
Vijana wakipanga kuni tayari kwa kuanza kuchoma
Go ahead
Vijana wakiweka moto baada ya kupata ruhusa kutoka kwa wanafamilia
Mwanaye Loose akiangalia moto kwa uchungu
Caroline akiwa haamini kwamba ndiyo mwisho
wa maisha ya mwanadamu aliyempenda
Dr. Philip Nelson alijiua kwa kujirusha kutoka karika ghorofa ya nne huko Oysterbay DSM tarehe 23/03/2013 na kufa papo hapo. Leo amezikwa kwa kuchomwa moto. Ni mara yangu ya kwanza kushuhudia maiti ikichomwa moto.
Ni kwa nini wameamua kumchoma moto?
1.Gharama za kumsafirisha kwenda Uingereza kumzika ni kubwa mara 20 ya kumchoma. Hivyo kwa kuzingatia hali yao ya kiuchumi, familia imeamua kumchoma, (cremate) na kupeleka majivu yake nyumbani badala ya mwili.
Nimejifunza jambo moja kutoka kwa familia hii, kwanza wamekuja watoto wawili tu, si kwamba hawapo wengine, ila gharama zisizo za lazima.
Pili, wametumia njia rahisi na nafuu ya kumzika ((cremation)
Nikajiuliza hivi inapotokea Mtanzania amefia China, Marekani........ tunatumia gharama kiasi gani kumleta hapa, na kisha kumsafirisha hadi shambani kwa baba yake kumzika?
Nikajikuta nakata shauri kwamba iliwa nimekufa sehemu ya mabali basi ni bora wanichome ili kuondoa usumbufu mwingi na gharama zisizo za lazima.
Utamaduni wa kuangalia gharama na usumbuufu mimi nimeuona ni mzuri. Ifike mahali makampuni ya kitanzaniza ya kuanzisha mazishi ya kuchoma (cremation) yaanza kufanya kazi. Hata kama mtu amefia hapa DSM awe na uwezo wa kuandika namna anayotaka azikwe au hata ndugu wawe na njia mbadala ya kuchoma. Nilivyoona, sio mbaya, na hasa ukizingatia gharama ni nafuu na muda mfupi.
Ndiyo maana nimeweka makala hii ili iweze kutufungua kutoka katika utamaduni wa mazoea na kuingia kwenye utamaduni mpya ambao kiukweli ni smart in terms of costs, time and efficiency.
Hata hivyo ni mara yangu ya kwanza kuhudhuria mziba wa rafiki ambaye hakuamini uwepo wa Mungu (atheist) Hakuna msalaba, hakuna biblia, hakuna msahafu hakuna chochote, wala sala zaidi ya kushika jeneza na kusema tu farewell/kwaheri. Baada ya mazishi niliuliza watoto kama walikuwa na dini yeyote na kkama hapana ni kwa nini? Walinijibu kuwa dini hazikuweza kuwapa majibu yanayoridhisha katika maisha yao. Kuwa dini zimekuwa chanzo cha mafarakano badala ya amani. Dini zimekuwa kama ngazi ya kuonyesha supremacy badala ya simplicity. Loose akaniuliza shwali, katika community unayoishi hakuna watu wanaoshika sana dini lakini wana visasi, chuki, na udhalimu mwingi? Nikamjibu wapo. Akaniambia kuwa yeye hajawahi kumdhulumu mtu, kumchukia mtu, kumwibia mtu, kumsaliti mumewe.......akataja kila aina ya dhambi ambazo hajazitenda and yet haendi kanisani wala msikitini, je dini ni nini? Jibu lake ni kwamba,
"My religion is just to be good"
Hata hivyo anaamini kuwa kuna supreme being ambaye ndiye anayemwezesha kuishi na anaamini kuwa baada ya kifo roho haipotei inaendelea kuwepo milele katika hali ya wema kama aliyekufa alikuwa mwema au katika hali ya mahangaiko a kutangatanga kama aliyekufa alikuwa mwovu.
Je, mtu anayejiua ana nafasi gani mbinginu (kwa supreme being)
Kwamba kama Dr. Philip ameamua kujiua, na kuwaaga ndugu na marafiki kwamba sasa basi, is a respective way of stopping making any more mistake. Is a honorable way of putting things to an end. And this is very common in Asia, Europe and America. And so everybody respect this decision even if you one does not like it.
MAY HIS SOUL REST IN PEACE WHEREVER IT GOES
Noma
ReplyDelete