Marais wa jumuiya ya Afrika
Mashariki wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka laiyekuwa Waziri wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda Marehemu Eriya Kategaya wakati
wa ufunguzi wa kikao cha kumi na moja cha Jumuiya hiyo jijini Arusha
leo mchana. Katika Hoteli ya Ngurdoto.Kutoka kushoto Rais Wa Burundu
Pierre Nkurunzinza,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri
Kaguta Museveni wa Uganda,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa
Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiteta jambo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati wa ufunguzi wa
kikao cha juu cha kumi na moja cha Wakuu wa nchi wa jumuiya ya Afrika
Mashariki kilichofaniyka jijini Arusha.
Marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye kikao cha kumi na moja cha Jumuiya hiyo jijini Arusha leo.
Baadhi wa ajumbe walioshiriki
ufunguzi wa kikao cha Juu cha kumi na moja cha Wakuu wa nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki(11th Extraordinary EAC Summit) kilichofanyika jijini
Arusha.Picha na Freddy Maro-IKULU
No comments:
Post a Comment