Mataifa yaliyoendelea ya G.20 yakaribishwa kuwekeza katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Viongozi
wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakiimba Wimbo wa Mataifa
hayo kabla ya kuanza kwa Mkutano wao wa 11 kwenye Hoteli ya Ngurdoto
Mkoani Arusha. Kutoka
Kushoto kuelekea kulia ni Waziri Mkuu wa Rwanda Bw. Pierre Damien
Habumuryemi, Rais wa Burundi Bw. Pierre Nkurunziza, Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Uhuru Kenyata wa
Kenya na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliyemuwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Sheni.
Rais
Uhuru Kenyata wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya akihutubia Mkutano wa Wakuu
wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza baada ya
Kuchaguliwa kuwa rais wa Kenya hivi Karibuni.
Baadhi
ya Mawaziri wa SMT na SMZ walioshiriki Mkutano wa Wakuu wa Mataifa ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye Hoteli ya Ngurdogo Mkoani Arusha
Tanzania. Kutoka kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais MBM Dkt.
Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mh. Fatma Abdullhabib Fejeji, Waziri wa Afrika Mashariki Mh.
Samuel Sita na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Tanzania Mh. Mahadhi Juma.
Mwenyekiti
wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Kaguta Museveni
aliyeshika Kofia akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake wa
jumuiya hiyo mara baada ya kumaliza Mkutano wao wa 11 wa Jumuiya hiyo
uliofanyika Ngurdoto Mkoani Arusha. Kushoto kwa Rais Museveni ni Rais
Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais Uhuru Kenyata wa Kenya na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyemuwakilisha Rais wa
Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Sheni. Kulia kwa Rais Museveni ni Waziri Mkuu
wa Rwanda Bw. Pierre Damien Habumuryemi pamoja na Rais wa Burundi Bw.
Pierre Nkurunziza.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwaongoza Wajumbe wenzake kutoka nje ya Ukumbi wa Mkutano wa 11 wa
Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mshariki mara baada wa kumaliza Mkutano wao
kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Ngurdoto Mkoani Arusha.(Picha na Hassan
Issa OMPR – ZNZ).
Mataifa
yanayoendelea kupiga hatua za haraka za Kiuchumi Ulimwenguni ya G. 20
yameshauriwa kuwekeza ndani ya Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) ili kuunga mkono harakati za Kiuchumi za Mataifa hayo.
Ushauri
huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri
Kaguta Museveni wa Uganda katika Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Jumuiya hiyo
uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kimataifa ya Ngurdoto iliyopo
Mkoani Arusha Tanzania.
Rais
Museveni amesema Mataifa hayo yenye muelekeo mzuri wa Kiuchumi yanaweza
kuongeza nguvu zao katika kusaidia miradi ya Miundo mbinu ya Barabara
,Mawasiliano na hata Sekta binafsi.
Amesema
Jumuiya ya Afrika Mashariki imelenga kunyanyua maisha ya Wananchi wake
kwa kuimarisha Sekta zisizo rasmi kwa vile uwezo wa Serikali hizo katika
kutoa ajira hasa kwa Vijana bado ni mdogo.
Mwenyekiti
huyo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ametolea mfano Taifa lake la Uganda
ambalo limejizatiti katika kuimarisha nguvu za sekta binafsi ili
kupunguza wimbi la vijana wengi wanaomaliza masomo yao ambao hubaki
wakizurura bila ya utaratibu wa kufanya kazi.
Akiwahutubia
Viongozi hao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao ni Rais Jakaya Mrisho
Kikwete wa Tanzania, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, Waziri Mkuu
wa Rwanda Bw. Pierre Damien, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi akimuwakilisha Rais wa Zanzibar pamoja na Watendaji wao
Rais Museveni amempongeza Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kwa kujumuika
pamoja katika mkutano huo baada ya kuchaguliwa kuiongoza Kenya.
No comments:
Post a Comment