ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, April 13, 2013

Viongozi mbali mbali wamuenzi Waziri Mkuu wa Zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (mwenye tracksuti ya bluu),Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala (wa tano kulia) na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro,Mh. Christopher Ole Sendeka,wakishiriki katika matembezi ya nusu kilomita ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 29 tangu kufariki kwa Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,yaliyofanyika jana huko Kijijini kwao Monduli Juu,Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,aliefariki miaka 29 iliyopita siku kama ya jana.
Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo,Dkt. Fenela Mukangala akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine.
Wake wa Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la Mume wao.
Mbunge wa Jimbo la Arusha,Mh. Godbress Lema akishiriki mbio za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine zilizofanyika kijijini kwake Monduni Juu,Mkoani Arusha jana.
Baadhi ya vijana wa jamii ya Kimasai wakikimbia mbio fupi za kumuenzi Waziri Mkuu wa zamani,Marehemu Edward Moringe Sokoine,kijijini kwake Monduli Juu,Mkoani Arusha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...