
Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi

Sehemu ndogo ya Fuso ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa.

Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Polisi vikiwa kazini

Mwili wa dereva wa lori moja kubwa
lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na askari jeshi, tayari
kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva huyu ametambulika kwa
jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa ndani ya gari hilo wakati
vijana wengine wakiendelea kupakia moram asubuhi ya leo

Kina mama wakilia kwa uchungu wakihofia kuondokewa na wapendwa wao

Hali ilivyo machimboni hapo

Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema asubuhi.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza
kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi la uokoaji na wengine
wakisubiri kutambua ndugu zao
No comments:
Post a Comment