Tanganyika ilipata uhuru wake Desemba 9/1961 na
ikapata kiti chake katika Umoja wa Mataifa Desemba 14, 1961. Namba ya
kiti hicho ni ‘GA resolution 1667 (XVI).’ Zanzibar nayo ikapata uhuru
wake Desemba 10, 1963 na ikapata kiti chake katika Umoja wa Mataifa
Desemba 16, 1963; namba ya kiti hicho ni ‘GA resolution 1975 (XIII).’
Ilipofika Aprili 26, 1964, mataifa hayo mawili
huru yaliungana na hapo ndipo ilipozaliwa nchi iliyojulikana kwa jina la
Tanzania.
Novemba 2, 1964 kupitia Wizara wa Mambo ya Nchi za
Nje ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliuandikia barua
Umoja wa Mataifa na kutaka Zanzibar na Tanganyika ziondoshwe katika
orodha ya mataifa na iingizwe nchi inayojulikana kwa jina la Tanzania.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na
muungano wa Siria na Misri walioungana mwaka 1958 na ni sawa na muungano
wa Yemen ya Kaskazini na Yemen ya Kusini walioungana mwaka 1990. Kwa
bahati mbaya muungano wa Siria na Misri ulivunjwa mwaka 1961 (ulidumu
kwa miaka 3).
Kwa sasa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
umefikia hatua nzuri na ya kupigiwa mfano duniani kwa sababu umedumu kwa
miaka 49 sasa.
Hata hivyo pamoja na kuwa muungano huu una muundo wa kipekee na kuwa umedumu kuliko miungano mingi iliyowahi kuwapo Afrika.
Muungano wa kwanza ulikuwa ni ule wa nchi za
Afrika Magharibi, mwishoni mwa miaka ya 50 na mwanzoni mwa miaka ya 60,
ulioanza na nchi mbili Ghana na Guinea na baadaye Mali ikajiunga nao.
Muungano huu ulitokana na vuguvugu la umajimui wa Afrika (Pan
Africanism), vinara wake wakiwa Kwame Nkrumah wa Ghana, Sekou Toure wa
Guinea na Modibo Keita wa Mali.
Novemba 1958 uliundwa muungano wa Ghana na Guinea
mara baada ya mkutano wa watu wa Afrika (All- African Peoples’
Conference). Ghana ilitoa fedha nyingi na kuipa Guinea ili ijitoe haraka
kutoka katika utegemezi wa Ufaransa.
Mei 1959 ikatangazwa kuwa umoja huo utatambulika kama Umoja wa Dola za Kiafrika.
Ilipofika Aprili 1961, Mali nayo ilijiunga na
umoja huo. Muungano huo ulivunjika mwaka 1962 kutokana na vita baridi,
ambapo Guinea ilionekana ikiinyooshea mikono Marekani wakati wenzake
walikuwa wakifuata mrengo wa kushoto wa Karl Marx/Lenin
Muungano mwingine wa nchi za Afrika ulifanyika mwaka 1981 baina ya nchi za Senegal na Gambia, uliojulikana kama Senegambia ambao ulikufa mwaka 1989.
Muungano mwingine wa nchi za Afrika ulifanyika mwaka 1981 baina ya nchi za Senegal na Gambia, uliojulikana kama Senegambia ambao ulikufa mwaka 1989.
Pamoja na kuwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar
ni muungano wa kupigiwa mfano, lakini bado si vyema kuacha kusema kuwa
una matatizo.
No comments:
Post a Comment