ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Sunday, May 19, 2013

Come Holy Spirit i need you now





Njoo Roho Mtakatifu ijaze mioyo na neema za umoja na mshikamano


Kanisa tangu mwanzo wake liliundwa kuwa la watu wote na litaendelea kuwa hivyo. Imesisiitiza homilia ya Baba Mtakatifu Benedikto XV1, kwa ajili ya Siku Kuu ya Pentekoste, iliyoadhimishwa na Mama Kanisa Jumapili iliyopita.

Papa akiuhutubia bahariya watu waliokusanyika katika Uwaja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa ajili ya kushiriki ibada ya Misa kwa ajili ya Siku kuu ya Pentekoste, alisema, tukio hili, huamusha upya ari za kujenga umoja na mshikamano kati ya mataifa.

Pentekoste ni utimilifu wa fumbo la Pasaka, Nguvu iliyowashukia mitume walipokuwa wamekutanika katika Chumba cha juu wakiwa na Bikira Maria Mama wa Yesu na wafuasi wengine. Ilikuwa ni siku ya kubatizwa kwa Kanisa, kubatizwa katika Roho Mtakatifu. Na aliendelea kuzungumzia wajibu wa nafisi tatu katika Utatu Mtakatifu, jinsi Roho Mtakatifu alivyounda Kanisa kama Kanisa la watu wote.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...