Padre akibariki akigeuza mkate na divai kuwa mwili na damu ya Yesu
Mwili wa Kristo
Padre akifanya mageuzo
Hostia ambazo hutengenezwa kwa ngano kabla hazijageuzwa kuwa mwili wa Kristo.
Divai inayotumika katika ibada ya misa takatifu
Venezuela imekuwa ikikumbwa na uhaba mkubwa wa vitu muhimu vya matumizi ya binadamu na hii ikitajwa kuwa ni kutokana na sera mbovu za chama tawala. Wiki iliyopita tulisikia kuwa Venezuela ilikumbwa na upungufu mkubwa wa toilet paper (karatasi za chooni). Sasa kanisa katoliki nchini Venezuela ambapo asilimia 90 ya wananchi wake ni waumini wa Kikatoliki limetangaza kuishiwa na divai ya altareni. Hii ni divai maalum inayotumika katika ibada za misa.
Uongozi wa kanisa katoliki nchini Venezuela umetahadharishwa kutumia kwa uangalifu mgao mdogo wanaoupata kwa matumizi hayo ya divai kwa ajili ya ibada ya misa takatifu. Hata hivyo upungufu huu ni pamoja na hostia ambazo hutengenezwa kwa unga wa ngano bila kutiwa amira kwa ajili ya mkate/comunyio wa altareni. Pamoja na upungufu huo, pia kuna upungufu wa vitu vingine muhimu kama kahawa, sukari na vyakula vingine muhimu sana. Wasambazaji wa divai ya altareni nchini Venezuela hawakupata mavuno mazuri msimu uliopita. Uagizwaji wa bidhaa hiyo ambayo inapatikana kirahisi sehemu nyingine duniani umekuwa mgumu kutokana na sera ya kikomunist na pesa ya nchi hiyo kukosa thamani.
Habari kutoka ndani ya kanisa hilo zinasema kuwa, uongozi wa kanisa umetoa ruhusa kutumika divai ambayo siyo ya altareni (non-sacramental wines) pale itakapotokea wameishiwa kabisa.
Hata hivyo, divai ya altareni (sacramental wine) sio divai ya kawaida. Hii ni divai maalum yenye kiwango kikubwa cha kilevi ambayo inafanya divai hii ikae muda mrefu bia kuharibika na haihitajiki kuwekwa kwenye friji.
Kwa hali hii, kanisa katoliki nchini Venezuela linapita katika wakati mgumu wa bidhaa hizi na bidhaa nyingine, hivyo huenda siku chache zijazi likatangaza kukosa mkate na divai ambavyo ni vitu muhimu sana katika kuadhimisha misa takatifu na bila hivi misa takatifu haitaweza kufanyika kabisa.
No comments:
Post a Comment