Januari Makamba atembelea jela ya mzee Mandela
Leo
nimetembelea Jela ya Robben Island, aliyofungwa Mzee Mandela kwa miaka 27.
Pichani ni chumba kidogo (cell) akichokuwa anaishi. Picha nyingine ni Mzee
aliyekuwa pia mfungwa kwa miaka mingi ambaye ndiye alinitembeza hapa na kunipa
historia. Nimekuja huku kwa mafunzo ya ziada ya uongozi, chini ya taasisi ya
African Leadership Institute chini ya mpango wake wa Archbishop Tutu African
Leadership Fellowship. Natumia fursa hii kutafakari na kujitathmini na kujifunza
kuhusu masuala ya Uongozi. Mifano ya viongozi kama Mandela na Nyerere ni muhimu
katika zoezi hili. Kizazi chetu cha viongozi wa Africa lazima kionyeshe ujasiri
wa vitendo na sio blah blah na kuuchukulia uongozi kama dhamana na kama wajibu
na sio kama zawadi wala fursa ya kujitajirisha au kujitengenezea sifa, umaarufu
na ufahari
No comments:
Post a Comment