Askofu wa Kanisa Katoliki,Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Pengo alisema hayo jana katika Kanisa la Mtakatifu
Joseph alipokuwa akitoa sakramenti ya kipaimara na aliwataka wasiwe na
hofu lakini waendelee kumwamini Yesu Kristo kama Mwana wa Mungu.
“Tuendelee kwenda makanisani,kamwe tusiogope
kuuawa,tuwe na imani kwamba Yesu Kristo ndiye mlinzi wetu na ndiye
atuongozaye,”alisema Pengo.
Kardinali Pengo alisema hata kama vyombo vya dola
vitakuwa vimeshindwa kuwalinda,waumini kamwe wasiache kwenda makanisani
kwa ajili ya kuabudu.
Pengo aliwataka waumini hao kutolipiza kisasi
kutokana na mauaji yaliyotokea hivi karibuni mkoani Arusha kwani kufanya
hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya Yesu Kristo.
“Wakristo kulipa kisasi ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya kikristo na sheria za nchi,” alionya Pengo.
Kauli hiyo imekuja baada ya watu watatu kuuawa kwa
bomu na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa hivi karibuni katika Kanisa
Katoliki,Parokia ya Joseph Mfanyakazi,Olasiti nje kidogo ya jiji la
Arusha.
Mauaji hayo yalitanguliwa na kuuawa kwa Padri
Evarist Mushi aliyeuawa Februari 17 wakati akielekea katika Kanisa la
Mtakatifu Theresia,Zanzibar kuendesha misa.
Pia Desemba 25 mwaka jana,Padri Ambrose Mkenda
alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi watu wasiojulikana wakati akisubiri
kufunguliwa geti nyumbani kwake Zanzibar.
Pengo aliwataka waumini wote kuendelea kusali kwa imani yao na kwamba matatizo yanayojitokeza yasiwakatishe tamaa.
Alisema hata katika mafundisho, kuna mambo mengi
ambayo yalifanywa na baadhi ya watu ili kumkatisha tamaa Yesu Kristo
asitimize malengo yake lakini baadaye alishinda.
“Vivyo hivyo waumini yanayojitokeza hivi sasa
yasitukatishe tamaa tuendelee na utaratibu wetu wa siku zote na
tutashinda,”alisema Pengo.
No comments:
Post a Comment