katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akisindikizwa na askari muda mfupi baada ya kuachiwa
katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda Akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari!
Mhadhiri Maarufu wa Kiisilamu Sheikh Habibu Mazinge (suti nyeusi) akimlaki Sheikh Ponda mara baada ya kuachiliwa huru.
Ponda akizungumza na waandishi wa habari.
katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akitoka nje ya jengo la mahakam ya hakimu mkazi kisutu
Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia nduguyake kutokana na kushinda kesi hiyo.
Waumini wa Kiislamu wakiwa
Wammbeba Juu mmoja wa aliyekuwa mshtakiwa mwenza na Shekhe Ponda Mara
baada ya Kuachiwa Huru leo Katika Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Waandishi nao walifanya mahojiano na baadhi ya washtakiwa na ndugu wa washtakiwa hao.
Akaingia kwenye gari!
Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari yoyote ambayo ingeweza kujitokeza
Ulinzi wa Ponda wakati wa kuondoka mahakamani hapo baada ya kuachiliwa.
Msafara ukavamiwa na wafuasi baada
ya dereva wa gari lake kusimamisha awasalimie wafuasi hao jambo ambalo
polisi walikuwa hawalitaki na kuzua mabishano mazito kwenye mataa ya
Maktaba Square.
Wafuasi wakivamia gari kumsalimia baada ya dereva wa gari hilo kulisimamisha huku polisi wakimvamia aliondoe gari hilo haraka.
Wafuasi wakajimwaga barabarani.Picha na Habari na Mdau Audifance Jackson
--
HATIMAYE katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasi wake 49
leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili na
kuonekana hawana kesi ya kujibu. Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa
kifungo cha Mwaka Mmoja nje kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa
na nia yakutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyo
mahakamani hapo paliibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi
wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.
Pamoja na maelezo yote aliyoeleza
Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja
kinachodaiwa na waisilamu hao.
1.Mahakama hiyo haina uwezo
wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro
ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo la umiliki.
2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai
mali hiyo waislamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi
wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
5.Upande wa mashtaka umeshindwa
kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa
sheikh Ponda. Awasihi Waislamu kufuata taratibu za kisheria ili kuipata
mali hiyo halali itumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
No comments:
Post a Comment