ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, May 14, 2013

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MANZESE WALIOVAMIWA NA MASHETANI LEO ASUBUHI


Wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese iliyopo Manzese Uzuri, jijini Dar es Salaam wamevamiwa na mashetani na kuanguka hovyo darasani huku wakipiga kelele na kuongea maneno yasiyoeleweka na kusababisha hofu kutanda maeneo hayo.







Tukio hilo limetokea kuanzia saa nne asubuhi ambapo alianza mwanafunzi mmoja kupiga kelele na kuanguka wakati wakiendelea na masomo ambapo alitolewa nje ya darasa lakini cha kushangaza waliendelea kuanguka wengine wengi huku wakipiga kelele na kupigana kama vichaa.
 
 
 Wanafunzi wa shule ya secondari manzese zaidi ya 30 muda huu wanaanguka hovyo hovyo na kusema a mane no yasiyoeleweka kutokana na kinachohisiwa kuna nguvu za Giza zimetanda shuleni hapo huku wakijibamiza kwenye miti:
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese aliyeanguka na kuweweseka.Mpaka sasa haijafahamika chanzo cha wanafunzi wa shule hiyo kukimbia ovyo,kuanguka na kuweweseka.

Picha:Zainab Chondo wa ITV

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...