Waziri
Mkuu Pinda akizungumza mbele ya baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi
kipya/Filamu pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wadau wengine wa
sanaa waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema leo
mchana,mara baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali
iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa
upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba
na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini.
Mh.Pinda
aliishukuru kampuni ya Clouds Media Group kwa kazi nzuri walioianzisha
ya kuwasaidia vijana kwa namna moja ama nyingine katika suala zima la
kuwaamsha na kuwafungua macho na kuwaelimisha namna ya kuziona fursa
zilizopo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha,aliongeza kuwa kupitia ujumbe
huo wa MADE IN TANZANIA kinachohitajika sasa ni kupanga ratiba nzuri ya
kuliendeleza zoezi hilo ikiwemo pia kwa kuzishirikisha taasisi nyingine
zikiwemo za serikali katika kuhakikisha jambo hilo linaendelea.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akiwakaribisha watu wote waliofika
kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Waziri
Mkuu Pinda.
Baadhi Wadau wa Muziki na Filamu wakiwa na mabango yao yaliyobeba jumbe mbalimbali mapema jana
kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda
fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa
hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga
uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa
Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea
Sehemu
ya umati wa watu ukiwa kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka
Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua
wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe katika
nafasi ya kujikwamua kimaisha,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia
wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na
kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea
Baadhi
ya Wasanii wa Filamu hapa nchini Wema Sepetu sambamba na shosti yake
Kajala walikuwa ni miongoni mwa wasaani waliounga mkono matembezi hayo
ya mshikamano yaliyokuwa yametawaliwa pia na mabango kadhaa yaliyobeba
jumbe mbalimbali za kupinga wizi wa kazi sanaa.
Matembezi
ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa
zilizopo,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa
nchini .
Baadhi
ya magari yakiwa yamesimama yakipisha matembezi ya mshikamano
yaliyokuwa yakielekea kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema jana mchana.
Baadhi
ya Watangazaji wa clouds FM,sambamba na wasanii wa muziki wa kizazi
kipya/tasnia ya filamu na wadau wengine wa sanaa wakiwa wamejumuika kwa
pamoja kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema jana mchana,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Mh Waziri Mkuu Pinda.
Mmoja wa Watangazaji wa kipindi cha Jahazi,Wasi Wasi Mwambulambo akiserebuka na Mh.Rehema Nchimbi.
Baada ya muda kulipita burudani ya pamoja ya mchanganyiko kama hivi safi kabisa kabla ya Waziri Mkuu kuwasili viwanjani hapo.
Pichani
kati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi,kulia mtangazaji wa
Clouds FM Mbwiga Mbwiguke na Shaffih Dauda (shoto) wakitwibiwirika kwa
pamoja mapema jana mchana mjini Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere skwea.
Mbunge
wa Jimbo la Kinondoni na Mdau mkubwa wa sanaa hapa nchini,Mh.Idd Azan
akiunga mkono harakati za kupapambana na maharamia wa kazi za sanaa hapa
nchini
Gari ya Waziri Mkuu Pinda ikiwasili
Waziri
Mkuu Pinda akisalimiana na Naibu Waziri wa Habari,Vijana, michezo na
Utamaduni,Mh.Amos Makala habari,Michezo mara alipokuwa akiwasili kwenye
viwanja vya Nyerere Skwea mapema jana mchana mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu Pinda akisalimiana na Mkurugenzi wa Vipindi na utafiti wa Clouds
Media Group,Ruge Mutahaba mara alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya
Nyerere Skwea mapema jana mchana mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu Pinda akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,mjini Dodoma
mapema leo mchana huku akiwapungia mkono baadhi ya wasanii wa muziki wa
kizazi kipya/Filamu pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wananchi
wengine kwa ujumla waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu
kabisa mapema jana mchana,mara
baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee
kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji
wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga
uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,pichani kati ni Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akimkaribisha. .
Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM (wote waliosimama nyuma).Reedio Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa TWENZETU kwa minajili ya kuielimisha jamii kuwa na tabia ya kupenda vya kwao na kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA kujikwamua kimaisha.
Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniii (wote waliosimama nyuma),mara baada ya kuzungumza nao kuhusiana na mambo mbalimbali juu ya sanaa ya Tanzania na namna ya kupambana na maharamia wa kazi zao,ambapo pia redio ya Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa Twenzetu kwa minajili ya kueilmisha jamii ya kupenda vya kwao kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA .
No comments:
Post a Comment