Jeshi
la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na
maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu
kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea
kwenye viwanja hivyo .
Kamanda Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.
Baadhi
ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa
jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee
Akizungumza
ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema
kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo
imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu
upelelezi.
Kamanda Sabas amedai kuwa jeshi la polisi liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.
Hali
kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi
wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya
kuomboleza ..
Hata
hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo
hilo na kuanza kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA ,
hali iliyoleta mvutano kati ya
viongozi wa jeshi la polisi na wafuasi hao.
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja alijichanganya na kuingia
katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu
wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.
Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi
kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke,
baada ya dakika kadhaa
mabomu yalianza kusikika.
Wakati huo huo, Tundu Lissu na Mustafa Akunai wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa
sasa. Hii ni taarifa toka kwa kamanda wa mkoa wa Arusha Liberatusi Sabas
akihojiwa na radio ya hapa jijini radio Sunrise fm..Kamanda Liberatusi
amesema makosa ya Wabunge hao ni haya:
Mkusanyiko usio rasmi
Kufunga barabara
Kuwashambulia polisi
Kamanda amesema watashikiliwa na jeshi la polisi mpaka uchunguzi utakapo kamilika. Hilo ndilo linaloendea mpaka sasa. Hizi ni habari sahihi zilizotolewa na kamanda wa mkoa huu wa polisi Liberatus Sabasi.
Mkusanyiko usio rasmi
Kufunga barabara
Kuwashambulia polisi
Kamanda amesema watashikiliwa na jeshi la polisi mpaka uchunguzi utakapo kamilika. Hilo ndilo linaloendea mpaka sasa. Hizi ni habari sahihi zilizotolewa na kamanda wa mkoa huu wa polisi Liberatus Sabasi.
No comments:
Post a Comment