ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, June 19, 2013

Ghana yawafukuza Wachina zaidi ya 200



  
Sehemu ya wachina Ambao ni wachimbaji haramu wa Dhahabu waliokamatwa huko Ghana na kurudihwa China
Baadhi ya wachimbaji haramu baada ya kukamatwa na jeshi la Ghana 
  
Wachimbaji haramu wakijaribu kuwarushia risasi maofisa wa Serikali wa Ghana walipokuwa wakiwasaka
 
Wachimbaji haramu wa Kichina huko Ghana
 
Ugomvi kati ya wachimbaji haramu wa Kighana na kichina ni kawaida na kuuana mara kwa mara
 
Wachimbajiharamu wakiandaliwa tayari kusafirishwa kwao China
 
Wachimbaji haramu wakitiwa ngucuni baada ya kurudihwa China



Nchi ya Ghana imefanya msako mkali uliopelekea kukamatwa kwa raiya zaidi ya 200 wa Kichina waliokuwa  wakifanya biashara haramu ya kuchimba dhahabu.
Kukamatwa kwa raia hao wengi wa kichina kumekuwa gumzo kubwa ulimwenguni na hasa bara la Afrika ambalo limeshuhudia ongezeko kubwa sana la raia wa Kichina ambao wanafanya biashara yeyote hata zile ndogo ndogo ambazo wazawa walikuwa wakizifanya.
Hata hivyo serikaki ya China imesema kwamba kukamatwa kwa raia hao hakutaathiri uhusiana uliopo kati ya Ghana na China. China inaliona Bara la Afrika kama mhilili mkubwa kwa ajili ya mali ghafi za viwanda vyake na mafuta.
Xuejum Oiu afisa katika wizara ya mambo ya nje ya China alisema kuwa uhusiano wan chi hizo mbili utaendelea kuimarika pamoja na kuwepo kwa hali hiyo ya raia wake kufanya uhalifu wa namna niyo huko Ghana, kufuatia msafara wake ulioenda Ghana kukutana na Rais John Mahama kujaribu kumaliza tatizo hilo.
Maofisa wa Ghana walifanya msako mkali mwezi huu na kuwakamata Wachina 202 ambao walikuwa wakichimba madini bila vibali. Maofisa hao walishafanya msako kama huo mara kwa mara lakini haukuwa mkubwa hivi. Wachimba madini hao wengi wao ni kutoka Shan Lin huko Guangzi Zhang kusini mwa China ambamo serekali ya china haijawapa kimaumbele kama sehemu nyingine.
Msemaji wa Serikali wa Ghana amesema kuwa raia 218 walisharudishwa kwao na sasa hawataruhusiwa tena kuingia Ghana “prohibited immigrants”
Mamia ya raia wengine wa China wanatarajiwa kuondoka wenyewe kwa hiari, ingawa chanzo cha habari hakijafafanua ni kwanini.
Uongozi wa Ghana umesema kwamba ukamataji huo haukuwahusisha Wachina peke yao lakini msako huo unatokana na hofu kwamba taifa kubwa la kichina kwa kutumia uweza wake wa kifedha litaweza kumeza uchumi wa taifa la Ghana. Ghana ni kati ya mataifa machache ya Afrika linaloonyesha uchumi imara na uchumi unaokuwa kwa kasi kubwa sana.  Ghana hata hivyo ni ya pili kwa uchimbaji wa dhahabu kwa wingi duniani. Kampuni kubwa kabisa inayojulikana kama AgloGold Ashanti inayochimba katika eneo la  Obuasi likiwa eneo lenye dhahabu nyingi mno.
 Biashara kati ya Ghana na China inafikia dola za kimarekani 5.43 bilioni. Ufanyaji wa biashra haramu umeelezewa kuweza kuharibu uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili.
Ninaipongeza serikali ya Ghana kwa kuthubutu na kuweza kufanya ilichokifanya.  Hapa Tanzania, Wachina wamezagaa kila kona, wanafanya biashara nyingi ambazo hata huwezi kuamini kama  kweli wamepata kibali cha kufanya hivyo. Pamoja na kuwa na ufanisi katika shughuli zao, tukumbuke kwamba fursa za kibiashara za wazawa zinasibwa kwa kuwa ni vigumu kuwa na ushindani hata kama tuko kwenye soko husia. Sidhani kama  kituo cha uwekezaji kinakubali kumsajili mwekezaji wa kichina anayekuja kuuza mitumba, viatu………. Na kusamehewa kodi. Mimi ni mmoja wa wafanya biashara ambao waliwahi kusafiri  kwenda China na kufanya biashara. Kwa sasa nyingi ya biashara zile zimekuwa ngumu kwa kuwa wa Wachina wenyewe wamekuwa maajenti na wauzaji. Unienda kariakoo sasa utakuta Mtanzania anauza nguo, na mchina anauza nguo zile zile. Tofauti ni kwamba mchina ndiye mwenye kiwanda na muuzaji na hapo hapo anakuja kama mwekezaji hivyo ana unafuu Fulani wa kodi. Matkeo yake  Mtanzania atashindwa kwenye ushindani usio sawa wa kibiashara Mchina atanawiri. Vivyo hivyo kwenye magereji………………….
Tufike mahali tuweke uzalendo mbele, tulinde mali zetu na biashara za watu wetu. Majuzi tu wamekamatwa na udongo huko kanda ya ziwa (kimya) wengine unasikia wamekamatwa na pembe za ndovu (kimya) Siku si nyingi wataanza kuuza hadi karanga mitaani na kahawa za mia mia, sisi tumekaa tu kimya.
Ghana wametuonyesha mfano tuige mfano huo ili kulinda rasilimali zetu na biashara zetu kwa ustawi wa nchi yetu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...