Msanii wa muziki wa kizazi Langa Kileo amefariki dunia jioni
ya leo katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua ugonjwa wa Malaria. Langa
ambaye aliingia rasmi kwenye muziki baada ya kuwa mmoja ya washindi Coca Cola
Pop Star, ambapo aliunda kundi la WAKILISHA kwa pamoja na Shaa pamoja na
Witness. Walifanikiwa kutoa nyimbo kadhaa ambazo zilitamba sana kwenye vituo
vya Radio na Television
Afisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel
Aligaesha amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa
kumi na moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo
kutokana na sababu za kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali hawawezi
kusema rapper huyu alikua anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya
hivyo.
Kwenye maelezo aliyoyatoa kwa millardayo.com Aminiel amesema Marehemu Langa alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa kuamkia jana (juzi)na kupatiwa huduma ambapo leo (jana) June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia.

Katika hatua nyingine, Baba wa marehemu Mzee Kileo amesema
kuwa mtoto wake Langa amefariki dunia jana majira ya saa 10 katika hospitali ya
Taifa Muhimbili.Taarifa kamili na mipango ya mazishi zitatolewa pale vikao vya
familia vitakapofanywa.Pia baba yake alisema msiba huu umetokea wakati mama
yake Langa hayupo Tanzania,alisema kwa sasa mama yake Langa yupo Marekani
lakini baada ya kupewa taarifa hizo tayari ameshakata tiketi ya kurudi Tanzania
na ataanza safari leo. Msiba uko nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni
No comments:
Post a Comment