Mama Salma Kikwete Mke wa rais wa Tanzania
Laura Bush Mke wa rais wa zamani wa Marekani George Bush
Michele Obama, mke wa rais wa Marekani Barrack Obama
Cherie Blair, Mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair
Maria da Luz Dai Guebuza, Mke wa rais wa Msumbiji
Janeth Museven, Mke wa rais wa Uganda
Sia
Nyama Koroma, mke wa rais wa Siera Leon
Dar es Salaam. Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush na
mkewe,Laura wanatarajiwa kuendesha Mkutano wa Kimataifa wa wake wa
marais wa Afrika kuzungumzia nafasi ya wanawake kuinuka kimaendeleo
utakaofanyika Dar es Salaam, Julai 1-2 mwaka huu.
Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyika nchini,
utakwenda sambamba na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama pia
utajumuisha maofisa wa Serikali,viongozi wa mashirika ya kiraia na
wasomi wa kada mbalimbali.
Taarifa iliyotolewa na Wakfu wa George W. Bush
imesema kuwa mkutano huo utakaokuwa na kauli mbiu; “Kuwekeza kwa
wanawake kunaiinua Afrika” imewataja baadhi ya wazungumzaji kuwa ni
pamoja na Bush mwenyewe na mkewe Laura, Mke wa Rais wa Marekani,Michelle
Obama, Mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza,Cherie Blair na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi
(Unaids), Michel Sidibé.
Taarifa hiyo imesema kuwa wake hao wa marais wa
Afrika wanatoa mchango mkubwa wa kusukuma mbele agenda za maendeleo
katika sekta za afya na elimu hivyo kukutana kwao kutatoa fursa nyingine
ya kujadiliana changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya pamoja.
“Wake za marais wanalo jukumu muhimu kuhusiana na
uboreshwaji wa ustawi wa wanawake… wao wana nafasi kubwa ya kuinua na
kuboresha sekta kama elimu,afya na maendeleo ya kiuchumi hivyo kukutana
kwao ni hatua muhimu itayotoa mwanga kuhusiana na hatua zinazopaswa
kufanywa kuwawezesha wanawake,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Baadhi ya wake za marais watakaohudhuria mkutano
huo ni wa pamoja na Mke wa Rais wa Uganda, Janet Museveni,mke wa Rais wa
Msumbiji, Maria da Luz Dai Guebuza, mke wa Rais wa Sierra Leone, Sia
Nyama Koroma na mwenyeji wao Salma Kikwete.
Miongoni mwa mada zinazotarajiwa kujadiliwa wakati
wa mkutano huo ni pamoja na kuwawezesha wanawake ujasiriamali kupitia
mafunzo ya teknolojia,kutoa fursa na kuboresha shughuli za kilimo kwa
wakulima wanawake na ukoaji wa maisha kwa kukabiliana na saratani ya
ziwa.SOURCE MWANAINCHI
No comments:
Post a Comment