
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya
Arumeru, Devotha Kamuzora jana alimkabidhi hati ya mashitaka
yanayomkabili, Victor Ambrose (20) ambaye ni mtuhumiwa pekee aliyepandishwa
kizimbani baada ya kutokea shambulio la bomu katika Kanisa la
Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti jijini Arusha.
Ambrose alikabidhiwa hati hiyo ya
mashitaka yanayomkabili jana katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru jijini Arusha
na kuambiwa na wakili wa Serikali, Adelaide Kasala kuwa
upelelezi dhidi ya kesi hiyo, haujakamilika na kumuomba Hakimu Kamuzora
kutaja tarehe nyingine.
Hakimu Kamuzora kabla ya kuahirisha
kesi hiyo alimuuliza Ambrose kama alipewa hati yake dhidi ya mshitaka
yanayomkabili. Ambrose alipojibu, “hapana.” Baada ya jibu hilo,
Hakimu alitoa hati
hiyo na Ambrose kukabidhiwa na kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 24.Ambrose
ambaye ni dereva wa bodaboda na mkazi wa Mrombo jijini Arusha, mara ya kwanza
alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Arusha na baadaye kuhamishiwa
Mahakama ya Wilaya ya Arumeru na kusomewa mashitaka yake kwa mara ya tatu sasa
huku akitakiwa kutojibu lolote, kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na
uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji.
Wakili wa Serikali, Adelaide
Kasala alidai mahakamani hapo Victor alitenda makosa hayo Mei 5, mwaka
huu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti jijini.
No comments:
Post a Comment