ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Tuesday, June 25, 2013

Tamko Kutoka Jeshi la Polisi Nchini Juu ya Taarifa za Upotoshaji Zilizofanywa na Mtangazaji wa Televisheni ya Channel 5 EATV Joyce Kiria Za Kuomba Msaada Kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili kusaidiwa na kujua aliko mume wake Henry Kileo ambaye ni Katibu Wa Chadema mkoa wa kinondoni na Kanda maalum ya Dar es Salaam


Mtangazaji wa televisheni ya Channel 5 EATV Joyce Kiria akiwa amewashikilia watoto wake Lingatone Kileo kulia na Lincorn wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo na kupaza sauti kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili kusaidiwa na kujua aliko mume wake Henry Kileo ambaye inadaiwa amepelekwa Igunga akituhumiwa na kesi huko Joyce Kiria amesema mpaka sasa hajaambiwa kama mume wake yuko wapi hivyo hata kama ana makosa anaomba afahamishwe kwani hajui kinachoendelea mpaka sasa.Picha na John Bukuku
Advera Senso Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania
--
 Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu 
Imetolewa na
 Advera Senso 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania
 

Huyu ndo MME WA JOYCE KIRIA NA VIJANA WENGINE WACHADEMA WAKIWA NA PINGU,KESI YA UGAIDI IGUNGA

Bw.Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza 

 Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za
uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.


Kamanda Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na wtuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...